• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

Kilimo

Maeneo yenye fursa za  kibiashara katika sekta ya kilimo

Asilimia 97  ya wakazi wa wilaya ya Igunga wanategemea sana kilimo kama shughuli kuu ya kiuchumi na kujiongezea usalama wa chakula.

 

Fursa za kibiashara katika mazao mchanganyiko

Wilaya ya Igunga inazalisha mazao ya chakula na biashara. Mazao ya chakula ni mahindi, mpunga, muhogo, viazi vitamu, mtama na mikunde. Mazao ya biashara ni pamba, alizeti, karanga,ufuta, choroko na korosho

 

Fursa za kibiashara katika mazao mchanganyiko 

Wilaya ya Igunga inazalisha mazao mengine ya biashara ukiacha zao la mpunga na pamba ambayo yanaweza kufanyiwa uwekezaji wa kibiashara na yakaleta tija kwa maendeleo ya wakulima na wilaya kwa ujumla wake. Mazao hayo ni alizeti, choroko na ufuta

 

Jedwali: Uzalishaji wa mazao haya kwa misimu 2014/2015 hadi 2017/2018

MSIMU

Mazao

Alizeti 

(tani)

Choroko 

(tani)

Ufuta

 (tani)

2014/ 2015

2,548

11,199

2,024

2015/ 2016

4,976

13,502

1,480

2016/ 2017

2,104

2,934

1,989

2017/2018

6,080

2,792

2,512

 

Fursa za kibiashara zinazotokana na mazao ya alizeti, choroko na ufuta

  • Kuweka viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti na ufuta
  • Kuwekeza katika vituo vya kununulia mazao mchanganyiko katka vijiji wilayani kote yanakolimwa mazao haya.
  • Kuweka viwanda vya kuongeza thamani ya zao la choroko.
  • Kuanzisha viwanda vya kutengeneza vyakula vya mifugo.

Vivutio vya kibiashara

  • Uwepo wa umeme wa grid ya taifa ambao umefika hadi vijijini
  • Uwepo wa barabara kuu ya lami inayoenda mikoa ya jirani na nje ya nchi
  • Barabara za vijijini (feeder roads) zinazoendelea kuimarishwa na TARURA
  • Maji ya uhakika yatakayoletwa na bomba la ziwa Victoria
  • Uwepo wa taasisi za kifedha wilayani Igunga
  • Uwepo wa amani na usalama katika Wilaya

Fursa za kibiashara katika zao la pamba

Wilaya ya Igunga ndiyo inaongoza kwa uzalishaji wa pamba katika mkoa wa Tabora. Asilimia 94 ya pamba yote inayozalishwa mkoani Tabora inatoka wilaya ya Igunga. Eneno linalolimwa pamba hapa wilayani limekuwa likiongezeka kila mwaka ingawaje mavuno yake yamekuwa yakiathiriwa na hali ya ukame na mlipuko wa wadudu/ magojwa ya mimea.

 

 Uzalishaji wa pamba wilayani igunga misimu ya 2014/2015 hadi 2017/2018

Jedwali : Uzalishaji wa zao la pamba msimu 2013/14 hadi 2017/2018

MSIMU

LENGO    (Ha)

UTEKELEZAJI (Ha)

UZALISHAJI (Tani)

2013/2014
          24,020
           22,550
                  17,700
2014/2015
          24,020
           21,112
                  16,100
2015/2016
          24,020
           22,180
                  10,900
2016/2017
          24,020
           18,440
                  10,700
2017/2018
          33,330
           56,608
                  16,400

Kielelezo: Uzalishaji wa zao la pamba ukilinganisha na malengo, utekelzaji na uzalishaji

Kutokana na uwezo wa kuzalisha pamba kwa kiasi kikubwa, fursa za kibiashara katika sekta ndogo ya pamba ni kama ifuatavyo:-

  • Kujenga viwanda vya kuchambua pamba ukizingatia viwanda 2 vilivyopo vinasaidiwa na viwanda vilivyoko nje ya wilaya ya Igunga  Viwanda hivi ni vile vya kuchambua pamba  (ginning), kukamua mafuta ya pamba (oil mills) na kutoa mbegu manyoya (delinting) ukizingatia Igunga ni kitalu cha taifa cha kuzalisha mbegu hapa nchini.
  • Eneo la wilaya lina fursa ya upatikanaji wa pamba kwa ajili ya viwanda vya kusokota nyuzi na kufuma nguo.
  • Viwanda vya utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na nyuzi za  pamba kwa ajili ya matumizi ya tiba na usafi
  • Kuwekeza katika zana za kilimo kwa kuziuza, kukodisha na kukopesha kwa wakulima.
  • Uzalishaji wa zao la Pamba
  • Ujenzi wa maghala
  • Usafirishaji na Ununuzi wa pamba

Vivutio katika kibiashara

  • Uwepo wa umeme wa grid ya taifa ambao umefika hadi vijijini
  • Uwepo wa barabara kuu inayoenda mikoa ya jirani na nje ya nchi na zile  za vijijini (feeder roads) zinaendelea kuimarishwa na TARURA
  • Maji ya uhakika yatakayoletwa na bomba la ziwa Victoria
  • Taasisi za kifedha zipo wilayani Igunga
  • Vyama vya msingi vya Ushirika 41 vyenye wakulima wanaolima maeneo makubwa ya pamba.
  • Uwepo wa wataalam wa kilimo kwa ajili ya huduma za ugani kwa wakulima
  • Uwepo wa amani na usalama katika Halmashauri ya Wilaya.

Fursa za kibiashara katika kilimo cha umwagiliaji

Halmashauri ya wilaya ya igunga ina eneo la jumla ya hekta 11,547  zinazofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji. Maeneo ambayo yamebainishwa kwa ajili ya uwekezaji wa  kibiashara wa kilimo cha Umwagiliaji kwa uzalishaji wa zao la mpunga ambalo ndiyo zao la kipaumbele linalofaa kwa chakula na biashara hapa wilayani yana eneo la hekta 8,097. Mchanganuo wa maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa kibiashara wa kuzalisha zao la mpunga kwa njia ya umwagiliaji ni kama ifuatavyo:-

Jedwali: Maeneo yanayofaa kwa kibiashara wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Igunga

Na
Kata
Kijiji
Zao linalofaa kuzalishwa
Eneo linalo hitaji kibiashara (ha)
Eneo lenye miundo mbinu   (ha)
1
Igunga
Mwanzugi

Mpunga

1,500

630

2
Igoweko
Buhekela

Mpunga

750

400

3
Igurubi
Igurubi

Mpunga

600

400

4
Choma
Choma

Mpunga

400

320

5
Mbutu
Mbutu

Mpunga

350

0

6
Isakamaliwa
Isakamaliwa

Mpunga

380

0

7
Simbo
Simbo

Mpunga

2,500

0

8
Kinungu
Mwamapuli

Mpunga

400

400

9
Igunga
Makomero

Mpunga

617

0

10
Mwashiku
Mwashiku

Mpunga

400

0

11
Itumba
Itumba

Mpunga

200

157

 
JUMLA
 
 

8,097

2,307


Aina ya fursa za kibiashara unaohitajika katika eneo hili la kilimo

  • Ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya zao la mpunga kwa lengo la kupata bei nzuri sokoni
  • Ujenzi wa viwanda vinavyotumia mali ghafi zinazotokana na masalia ya mpunga kama mkaa, mbao laini, chakula cha mifugo, samani n.k
  • Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji (kama mabwawa, mifereji, mabomba, mashamba/ plots) kwa lengo la kuongeza tija inayolenga uzalishaji zaidi kwa muda mfupi ili kuleta ufanisi kwa wakulima watakaolipia gharama za miundombinu na kuzalisha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya mpunga.
  • Ujenzi wa maghala makubwa ya kuhifadhia zao la mpunga kabla ya kuongezwa thamani na kupelekwa sokoni
  • Uuzaji wa pembejeo za kilimo kama mbolea , madawa na vifungashio katika maeneo yanayozalisha mpunga na mazao mengine.
  • Biashara katika zana za kilimo kama matrekta,mashine za kupandikiza mpunga, mashine za kuvunia mpunga na kuchakata mpunga kwa lengo la kuziuza au kuzikodisha kwa wakulima.

Maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha Umwagilaji

Ujenzi wa mabwawa makubwa

Miundombinu ya Umwagiliaji

Vivutio vya  kibiashara katika kilimo cha umwagiliaji  wa zao la mpunga

  • Uwepo wa Maeneo yanayofaa kwa umwagiliaji
  • Uwepo wa miradi mikubwa ya umwagiliaji
  • Uwepo wa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji zaidi ya hekta 8,097.
  • Uwepo wa umeme wa grid ya taifa ambao umefika hadi vijijini
  • Uwepo wa barabara kuu inayoenda mikoa ya jirani nanje ya nchi
  • Barabara za vijijini (feeder roads) inaendelea kuimarishwa na TARURA
  • Uwepo wa fursa kubwa ya kuvuna maji ya mvua kwa kukinga matuta makubwa (earthfill dams)
  • Uwepo wa mabonde makubwa yenye udongo wenye rutuba
  • Uwepo wa Taasisi za kifedha wilayani Igunga
  • Uwepo amani na utulivu katika Wilaya

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa