EQUIP- Tanzania watoa Mafunzo, kwa maafisa Elimu Kata juu ya Ufuatiliaji na tathimini ya mfumo wa Kiunzi cha Afisa Elimu Kata juu ya shughuli za kuongezea shule kipato, (income Generative Activity -IGA) na Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWW), ambayo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya Acacia Land kwa siku tatu na kuisha leo tarehe 11.08.2018, Igunga Mjini.
“Mwongozo huu utawasaidia kuweza kusimamia majukuu yenu pamoja na kuweza kujifanyia tathimini ya njisi unavyotekeleza majukumu yako katika kata yako”aliongeza. Bibi. Martha Bayo Mratibu wa EQUIP-Tanzania Wilaya ya Igunga,
Wakati huo huo baadhi ya Maafisa Elimu kata walioshiriki katika mafunzo wamesema wamepata vitu vipya pamoja na kuishukuru EQUIP-Tanzania, kwa mpango wao wa kuwaletea mfumo huo. Akiongea Afisa Elimu Kata ya Choma, Bwana Obrey Nickson Mwambipile amesema “nimefurahi kupata mafunzo haya kwani nimejifunza namna ya kufanya tathimini ya utendaji kazi wa walimu wakuu pamoja na namna ya kujitathimini Afisa Elimu Kata mwenyewe”
“Nimepata kujifunza na kuelewa juu ya kujaza kiunzi cha tathimini naufuatiliaji wa taarifa kwa njia ya mfumo pamoja na kiunzi cha taarifa za shule kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku na Shughuli za kuongezea shule kipato, (income Generative Activity -IGA) na Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWW )”ameongeza Bwana, David Joram Afisa Elimu Kata ya Lugubu.
Nae Mthibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Igunga Bwana Remigius Harara amewakumbusha Maafisa Elimu Kata kuendelea kuwa karibu na Walimu wakuu, waalimu na wazizi ili kuwezesha shule kujikwamua kwa kuendeleza miradi ya maendeleo katika shule zao ili kuondokana na hali ngumu na kuwahimiza watoto wao kwenda shule pasipo kutoroka kwa kufanya mikutano ya shule na wazazi.
Katika mafunzo hayo yaliyowafathiliwa na EQUIP_Tanazania, na kuendeshwa na Mthibiti ubora wa shule Wilaya ya Igunga na Mratibu wa EQUIP-Tanzania Wilaya ya Igunga, yamehudhuriwa na Maafisa Elimu Kata, ambao wamekiri kuwa wanakwenda kufanyia kazi Mfumo huo wa kujitathimini wenyewe pamoja na walimu wakuu ambao wapo katika maeneo yao ya kazi.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa