Mheshimiwa George Joseph Kakunda, Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na mamlaka za serikali za mitaa OR-Tamisemi, amewapongenza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Wataalam kwa kutekeleza Miradi kwa ubora na kusimamia pesa za Serikali vizuri katika ujenzi wa miundombinu ya maji Isenegeja na Mabweni katika shule za Sekondari ya Nanga na Ziba hivi karibvuni.
“Serikali ya awamu ya tano inawajali wananchi wake ndiyo maana inaleta Miradi kama ilivyo kwenye ilani ya chama tawala CCM” alisema Mhe. Naibu Waziri OR-Tamisemi.
Mhe. Naibu Waziri OR-Tamisemi aliwataka kutumia nishati ya umeme umeme kwani mradi wa Umeme vijijini REA wameelekezwa kufikisha umeme kwenye Miradi hasa ya maji ili kuwezesha miradi hiyo kuwa endelevu. Solar ni gharama zaidi, au unaweza usilete tija kwani unatengemea mwanga wa jua, Solar zilizonyingi huharibika mapema ndani ya miaka miwili aliwashauri kujifunza maeneo mengine katika mkoa wa Manyara ambapo wametekeleza Miradi ya maji.
Aliendelea kuwambia wananchi na watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa weledi na kusimamia miradi kikamilifu ili pesa zinazotolewa na Serikali zisipotee bali zilete tija na manufaa kwa watanzania kwa kukamilisha miradi kwa wakati na yenye ubora.
Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mhe.John Gabriel Mwaipopo Mkuu wa Wilaya ya Igunga alisema “Mhe.Naibu Waziri Wilaya ya Igunga imepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za sekondari kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo katika awamu mbili hadi sasa. Awamu ya kwanza tumepokea jumla ya Tshs. 316,000,000.00 zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu ya shule mbili za Nanga na Ziba Sekondari.”
Mhe.Mkuu wa Wilaya alisema katika fedha hizo zilizoletwa Nanga Sekondari ilipokea Tshs. 241,000,000.00 mnamo tarehe 05/07/2017 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni mawili (2) kwa Tshs. 150,000,000.00, vyumba vya madarasa vine (4) kwa Tshs. 80,000,000.00 na matundu ya vyoo kumi (10) kwa Tshs. 11,000,000.00.
Pia shule ya sekondari Ziba ilipokea tshs. 75,000,000.00 mnamo tarehe 12/09/2017 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja (1)
Katika awamu ya pili Wilaya ya Igunga imepokea tshs. 190,000,000.00 mnamo tarahe 29/12/2017 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Ziba kwa mchanganuo ufuatao; Ujenzi wa mabweni mawili (2)kwa Tshs. 150,000,000.00, na ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili 2 kwa Tshs. 40,000,000.00
Ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Isenegeja ulianza kutekeleza tarehe 28 Novemba, 2017 na utagharimu Shillingi Million mia tatu laki tano na ishirini na sita elfu mia mbili arobaini tu (300,526,240.00).Ambapo uchimbaji wa mtaro wenye urefu wa mita 7,912, ufungaji wa mabomba, Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 60,000 na lita 10,000, Ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji, ujenzi wa nyumba ya Mtambo na uzio.
Katika mradi wa maji Isenegeja ujenzi umefikia asilimia (37%), Ujenzi wa nyumba ya mtambo umefikia asilimia 70%, Ujenzi wa mlingoti (Riser)umefikia asilimia (50%).
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa