Mwalimu Saten Chalula, Afisa Elimu Maalum Wilaya ya Igunga, amewataka walimu wa madarasa ya utayari kutumia njia na mbinu mbalimbali za kufundishia na kujifunzia kuwasaidia watoto wa madarasa hayo ili kufikia asilimia 100% ya kuwawezesha kuwa tayari kuanza shule na kufaniwa kuwawezesha kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu KKK, alipowasilisha mada katika ukumbi wa Maxwell mjini Igunga hivi karibuni.
Aliendelea kusema madarasa ya utayari ni ya Muhimu sana kwani yanasaidia kukuza vipaji vya wanafunzi na kusaidia kujua kusoma mapema na wanafunzi hao kujipambanua mapema.
Mwalimu wa darasa la utayari toka shule ya Msingi Isakamaliwa Alex Machibya alikubali kuwa madarasa hayo yanachangamoto nyingi ambazo ni ukosefu wa majengo ya kudumu, kutokuwepo posho kwa wawezeshaji, ukosefu wa uji na wingi wa watoto vituoni. Baada ya hapo walikaa katika makundi na kujadili mafanikio yaliyofikiwa kwa madarasa hayo pamoja na changamoto na utatuzi wake.
Naye Mwalimu Salome Kidili, mwezeshaji angazi ya Wilaya ya Igunga aliwataka walimu hao kuendelea kujituma kwa kuwalea watoto hao na kuwajengea uwezo wa kujiamini ili waweze kufikia malengo yao hapo baadae.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa