• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

TANGAZO LA KAZI

16 July 2024

                   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

                                  OFISI YA RAIS
        TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 

               HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA

Simu:        +255 (026) 2650019 (G/L)                                                Halmashauri ya Wilaya,                                                                         

                 +255 (026) 2650021 (D/L)                                                16 Mtaa wa Bomani,                                                   

Nukushi:   +255 (026) 2650242                                                         45682 Igunga Urban.

Barua pepe:ded@igungadc.go.tz                                                      S.L.P. 19,

Tovuti: http://www.igungadc.go.tz                                                         IGUNGA – TABORA

Unapojibu Tafadhali taja:-                                   

Kumb. Na. AB.285/294/01/64                                                                   16 Julai, 2024

 

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-

 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI (15).

 

  • MAJUKUMU YA KAZI.
  • Kuwa Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji
  • Katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA MWOMBAJI

 

Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya jamii kutoka chuo cha Serikali za Mitaa au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

 Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II - NAFASI (05)

 

  • MAJUKUMU YA KAZI
  • Kuorodhesha  barua   zinazoingia   masijala   kwenye   Regista                           (Incomming Correspondence Register)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
  • Kutekeleza kazi zote atakazopangiwa na msimamizi wa kazi

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya masjala kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

 

 

DEREVA DARAJA LA II NAFASI (05)

 

  • MAJUKUMU YA KAZI
  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kufanya usafi wa Gari,
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

 

Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

 

Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ni TGS B

 

MASHARTI YA JUMLA

 

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CCA. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 Julai, 2024.

 

 

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

  •  
  •                                                    
  • MKURUGENZI MTENDAJI,
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA,
  • S.L.P. 19,
  • IGUNGA.
  •  

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

 

Limetolewa na:-

  • MKURUGENZI MTENDAJI,
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa