Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, ni moja ya Idara mtambuka ambayo lengo lake kuu ni Kusaidia jamii kutafsiri fursa na vikwazo vilivyopo katika mazingira yao na kutumia rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo. Utekelezaji wa malengo haya unaongozwa na Sera mbalimbali za Maendeleo ambazo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii ya 1996, Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000, Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya 2001, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007, Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya 2004 na Sera ya Taifa ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI ya 2001 na Sheria ya NGOs Namba 24 ya mwaka 2002.
Idara inatekeleza majukumu yake kulingana na dhana ya Maendeleo ya Jamii ambayo inaelezea hatua zinazowezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia rasilimali zilizopo kujitatulia matatizo hayo, kujipatia na kujiongezea kipato na kujiletea maisha bora zaidi na hivyo kwa ujumla, kujiletea maendeleo.
Katika utekelezaji wake Idara inaratibu mipango ya maendeleo ikiwa ni pamoja na utafiti, mipango na takwimu, masuala ya jinsia, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) kwa kushirikiana na Idara ya Afya, Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na uratibu wa asasi zisizokuwa za ki serikali (NGOs, FBOs & CBOs), vikundi vya kiuchumi vinavyotekeleza shughuli zake ndani ya Wilaya ya Igunga na Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii:
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa