Idara ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina jumla shule za sekondari 33 kati ya hizi, 29 ni za Serikali, 03 zinamilikiwa na taasisi za kidini, na 01 ni ya mtu binafsi. Aidha, kati ya shule 33 zilizopo wilayani Igunga shule 03 zina kidato cha tano na sita ikiwa 02 ni za Serikali na 01 ni ya taasisi ya Dini.
Idara ya Elimu Sekondari inaundwa na vitengo vitatu katika kutekeleza majukumu yake. Vitengo hivi ni kama ifuatavyo:-
IDADI YA WALIMU
Idara ya Elimu Sekondari inahitaji walimu wa sekondari 670 kwa ajili ya shule za sekondari za serikali, waliopo ni 415 hivyo kuna upungufu wa walimu 255.
IDADI YA WANAFUNZI
Idara ya Elimu Sekondari inawanafunzi wapatao 11539 ikiwa wavulana 5671 na wasichana 5868. Aidha, katika shule za sekondari za serikali kuna wanafunzi 9436 ikiwa wavulana 4778 na wasichana 4658. Katika shule za binafsi kuna wanafunzi 2103 ikiwa wavulana 893 na wasichana 1210.
MAJUKUMU MAKUU YA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa