Bi.Catherine Mathias Afisa mradi wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives), Wilaya ya Igunga kutoka shirika la Care International Tanzania amekabidhi vifaa vya kusaidia akina mama katika uzazi salama katika zahanati 16, kituo cha Afya 1, mbele ya Mkurugenzi Mtendaji na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, makabidhiano yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga hivi karibuni.
Bi.Catherine aliendelea kusema Shirika la Care Internation Tanzania kupitia mradi wake wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives) unafanya kazi katika kata 33 na vijiji 64 vya Wilaya ya Igunga. Kwa kupitia shirika la care international Tanzania, radi wa TAMANI umetoa vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ya mama na mtoto vyenye thamani ya shilingi milioni themanini na nane laki tano thelathini na tano mia sita tu. Tsh.88, 535,600.00
“ili kufikia lengo mradi umelenga mambo makuu mawili, ambayo ni kuboresha huduma kwa kutoa mafunzo na kuongeza huduma katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.” aliongenza Bi. Catherine.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashuri ya Wilaya ya Igunga Bwana Revocatus L.K.Kuuli, amewashukuru Care International Tanzania chini ya mradi wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives) kwa kutoa msaada mkubwa wa vifaa vya thamani ya Tsh.88,535,600.00, amendelea kuwaomba kusaidia Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pale watakapo fanikiwa tena.
Mradi umetoa mafunzo kwa hudumu wa afya ngazi ya jamii 130, ambao ndio kiunganishi cha jamii na Zahanati katika kutoa huduma nzuri ikiwa ni kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na watoto chini ya miaka mitano.
Nae Bwana Mayunga Nhondo Mayunga mratibu wa uzazi salama wa Mama na mtoto amewashukuru TAMANI(Tabora Maternal and New born Initiatives) kwa msaada walioutoa, ikwa ni pamoja na mradi kutoa mafunzo ya uzazi salama Basic emergency management of Obsteric and neonate Care (BemonC) kwa watumishi wa afya 30, na Comprehesice emergency Management of Obstetic and neonate Care (CemonC) kwa watumishi 5.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa