MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bi. Selwa Abdalla Hamid ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo.
Bi. Selwa amefanya ziara hiyo Ijumaa Januari 17, 2025 kwa lengo la kuhakikisha kila aina ya mradi unaotekelezwa unakamilika kwa wakati.
Alisema miradi mingi imetekelezwa vizuri, hivyo wanatarajia itaendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha, alitoa maelekezo kwa Wahandisi wa Halmashauri hiyo kuendelea kuwabana Wakandarasi kwa lengo la kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na viwango kulingana na thamani ya fedha.
Alihimiza kuwa Mkandarasi anatakiwa kuhakikisha anaongeza mafundi kwa lengo la kuongeza kasi kwa sababu miradi inahitajika ianze kutoa huduma.
Mbali na ukaguzi wa Miradi, Bi. Selwa alitembelea shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Nyandekwa na Igumila kwa lengo la kuona uhalisia wa kuripoti kwa wanafunzi wa darasa la awali, darasa lakwanza na kidato cha kwanza.
Katika ziara hiyo, Bi. Selwa aliambatana na Mhandisi, Dickson nkenja.
===== //// ===== ///// ==== ///// ====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa