Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Dr Charles Msonde amewapongeza Viongozi wa Chama na Serikali kwa ushirikiano walionao katika usimamizi wa miradi ya Elimu ya Shule za Msingi na Sekondari.Dr Msonde amesema Serikali inamalengo iliyojiwekea katika utoaji wa Elimu Nchini,ili Malengo hayo yatimie ni lazima kuwepo na Falsafa ya pamoja kati ya Viongozi wa Chama (CCM) na Viongozi wa Serikali.Ameyasema hayo 27/06/2023 akiwa kweye Ujenzi wa Shule Mpya yenye Mikondo 16 inayojengwa kwa Mradi wa BOOST.Pia Dr Msonde alitembelea Shule ya Sekondari Nanga na kuona ujenzi wa Madarasa na Mabweni kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha 5,mwaka 2023. Katika Mradi huo wa Mabweni na Madarasa Dr Msonde aliwataka Viongozi na Mafundi kufanya kazi usiku na mchana ili malengo ya Serikali ya kupokea Wanafunzi wa kidato cha 5 mwaka huu yatimie.
Msonde alieleza katika hutupa yake ya majumuisho katika Ukumbi wa Halmashauri kuwa,Miaka ya 2016 kunaongezeko kubwa la Wanafunzi wa Shule za Msingi,ongezeko hilo limefanya wanafunzi laki 4 na kidogo mwaka 2016 kujiunga na Kidato cha kwanza.
Mwaka 2021 wanafunzi laki 9 na 70 elfu (970,000) walijiunga na Kidato cha 4, Mwaka huu (2023) Wanafunzi Milioni 1 na 76 (1,000,076) walijiunga na kidato cha 4 hii inatokana na Sera ya Elimu inayosema Elimu Msingi hadi Kidato cha 4. Dr Msonde alisema kuwa idadi hiyo ni kubwa hivyo Serikali inayoongozwa na Mhe,Daktari Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuweka Miundo Mbinu toshelevu kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata Elimu Bora.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa