Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh.John Gabriel Mwaipopo amekuwa Mgeni Rasmi katika Harambee ya uchangiaji wa Ujenzi wa Vyumba Vitano vya madarasa katika Shule ya Sekondari Choma iliyopo Tarafa ya Manonga Kata ya Choma. Akiongea na wananchi pamoja na Wageni waalikwa Mgeni rasmi alisema “Elimu ndiyo itakayo wakoomboa na ndio urithi wa watoto wetu kwa kuwa tumeshiriki kuwaleta hapa Duniani ni wajibu wetu kuwalea na kuwatunza ikiwa ni pamoja na kusaidiana na Serikali yetu ya Jamuhri ya Muungano wa Tanzania kuimalisha miundombinu hasa madarasa”
Pia aliwaeleza wananchi kila Serikali inakuwa na vipaumbele hivyo ni wajibu wetu kama watanzania na watu wa Choma na Igunga kwa ujumla kuchangia maendeleo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Choma Mwl.Richard Rutandula akisoma taarifa fupi ya Shule ambayo ilionyesha mahitaji Makubwa ya shule hiyo alisema “ Ndg Mgeni Rasmi Shule ya Sekondari Choma ilianzishwa rasmi mwezi Mei, 2006 ikiwa na Vyumba vinne vya Madarasa tu, ni shule ambayo ujenzi wake sambamba na nguvu za halmashauri ya Igunga , Serikali Kuu pia nguvu ya wanannchi wa Kata ya Choma yenye Vijiji mama vitatu ambavyo ni Choma, Chibiso na Bulangamilwa”.
Mkuu wa Shule aliendelea kusema shule kwa ujumla wake inamapungufu mengi katiak maeneo mbalimbali kama vile Vyumba vya Madarasa mahitaji 17 yaliyopo 08, pungufu 09, Nyumba za waalimu mahitaji 14, zilizopo 03, Mapungufu 11, Mabweni Mahitaji 05, Zilizopo 01, pungufu 04, Maabara, Vyoo Mahitaji Matundu 30, vilivyopo 06, Mahitaji 24, pia madawati/Meza Mahitaji 679,yaliyopo 446, Mapungufu 233.
Hivyo aliendelea kutoa mchanganuo wa makisio ya ujenzi wa Vyumba hivyo vitano vya madarasa ambapo makisio ya gharama zote za ujenzi na ukamilishaji wa Vyumba hivyo ni Tsh.23, 823,700.00 (Shilingi milioni ishirini na mbili laki nane ishirini na tatu elfu mia saba tu).
Mh. Peter Onesmo Maloda Diwani Kata ya Choma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Igunga ambaye ndiye aliyekuwa mwenyeji wa Harambee hiyo aliongozana na Mh.Williamu Wales Jomanga Mwenyekiti halmashauri ya Mji Nzega,
Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Igunga Bw.Revocatus L.Kuuli pamoja na Afisa Elimu Sekondari Bw.Aloyce Kaziyareli walikuwepo katika harambee hiyo ambapo waliwawakiisha wakuu wa Idara na Vitengo. Pia Afisa Tarafa ya Manoga Bi.Maltha L.Tevely aliongozana na baadhi ya Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini.
Mgeni rasmi Mh.John Gabriel Mwaipopo (Mkuu wa Wilaya ya Igunga) akiongoza harambee hiyo aliweza kupata pesa taslimu kiasi cha (Tsh.230,000.00) shilingi laki mbili elfu thelethini tu, pamoja na ahadi (Tsh.2,975,000.00) shilingi milioni mbili laki tisa sabini na tano tu. Simenti mifuko 113, Bati bandali Moja, Nondo 04,Mchanga gari moja vyote vikiwa na jumla ya (Tsh.5,420,000.00) shilingi milioni tano laki nne ishirini elfu tu.
Mh.Mgeni rasmi aliwaomba na kuwaagiza Kamati ya shule na Mh.Diwani wa kata ya Choma Mh.Peter Onesmo Maloda ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga waendelee kuwahimiza wananchi kuchangia ujenzi huo ili wanafunzi waweze kupata madarasa ya kujifunzia.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa