Mkuu wa Shule Mwayunge Sekondari mwalimu Amithayori R.Nehemia, amefurahi kuwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2017, Wilayani Igunga alipokuwa anakabidhiwa tuzo ya Most Improved School (Shule iliyoongeza ufaulu kwa kiwango cha juu) katika ofisi za idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Igunga jana tarehe 09.01.2019.
Shule ya Sekondari Mwayunge imepata tuzo hiyo, miongoni mwa shule mbili nyingine ambazo zinazofanya vizuri kwa miaka miwili mfululizo ambazo ni Umoja Sekondari na St. Thomas Sekondari zilizopata Tuzo ya Shule zinazofanya vizuri sana (Best Performing School) hapa nchini Tanzania.
“Mwayunge Sekondari ilianzishwa mwaka 2011, ikiwa na wanafunzi 82 wa kiume 39 wa kike 43 ambao walihitimu kidato cha nne mwaka 2014. wa kiume 23 wa kike 9 na hakuna aliyeendelea na masoma ya elimu ya kidato cha tano, Mwayunge ina jumla ya walimu 22 wa kiume 12 na wa kike 10” ameongeza Mwl Nehemia Mkuu wa Shule.
Mwaka 2015 Shule ya Sekondari Mwayunge ilifanya vibaya katika mitihani yake ya kidato cha nne, kwa ushirikiano wa walimu na Idara ya Elimu Sekondari Wilaya ya Igunga. Mwaka 2016 Mwayunge Sekondari ilifanya vizuri na kupongezwa kwa kupatiwa cheti pamoja na fedha tasilimu Tsh.2,000,000.00 toka Wizara ya Elimu Sayansi naTeknolojia.
“Shule ya Sekondari Mwayunge imeendelea kuongeza bidii katika ufundishaji na ujifunzaji, ambapo kwa mwaka 2017 iliongeza ufaulu kwa kiwango cha juu,(Most improved School) ambapo tumepokea tuzo hii tukiwa miongoni mwa shule zilizoongeza ufaulu nchini kwa mwaka 2017”ameongeza Mwalimu Nehemia Mkuu wa Shule.
“Nampongeza Mkuu wa Shule na Walimu wote kwa kuongeza ufaulu,na kuwashauri waendelee kuongeza bidii ili ufaulu kwa mitihani ya kitaifa na mitihani ya ndani uongezeke zaidi pia kuwaimarisha wanafunzi kimaarifa na kuendelea kuiletea sifa Shule, idara ya Elimu Sekondari pamoja na halmashauri kwa ujumla”ameongeza Kaimu Afisa Elimu Sekondari Rashid Bundallah.
Mwayunge Sekondari ina Jumla ya wanafunzi 415, na inategemea kupoke wanafunzi 100 wa kidato cha kwanza mwaka 2019 ambao watafanya shule kuwa na wanafunzi 515. Kidato cha nne 2019 ni wanafunzi 93 wa kiume 41 na wa kike 52 matarajio ya walimu na mkuu wa shule ni kupeleka wanafunzi 35 kidato cha tano kwa 2020.
Shule inamafanikio iliyoyapata japo palipo na mafanikio hapakosi changamoto, Mwayunge Sekondari ina mapungufu ya nyumba za walimu 22, Jengo la Utawala pamoja na maabara zote tatu maabara ya Fizikia, Biolojia na Kemia.
Mkuu wa shule ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwezesha Shule kupata fedha za Elimu bure pamoja na kushirikishwa kufanya maamuzi katika ngazi za shule. Amewashukuru walimu wote kwa kuendelea kumpa ushirikiano katika kuendelea kuimalisha Mwanyunge Sekondari na halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Imetolewa na
Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa