MKUU wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Ndug. Hamisi H. Hamisi amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara na kupandisha watumishi vyeo.
Ndug. Hamisi ametoa shukrani hizo leo Septemba 15, 2025 wakati akiongea na watumishi kutoka katika Kata sita katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Bishop Batenzi Hospitali ya Rufaa Nkinga Kata ya Nkinga mjini hapa.
Amesema serikali inawapenda watumishi kwa sababu inafanya kila namna kuwapandisha vyeo.
Aidha, amewataka watumishi kupata ushauri wa kitaalamu wanapokuwa wanakwenda kusoma kwa lengo la kusoma kitu ambacho kitakua na tija katika maisha yao ya kiutumishi.
Akiongelea kuhusu makosa ya kinidhamu, amesema kutoroka kazini kwa siku tano, kutumia mali za ofisi, kutoheshimu viongozi, kuwa na kazi nyingine wakati wa muda wa kazi, kukataa uhamisho na kushindwa kutekeleza majukumu ya mwajiri.
Ameongeza makosa mengine ni kushindwa kutekeleza majukumu kwa sababu ya ulevi, kutoa siri za ofisi, kuto jali na kusababisha hasara kwa mwajiri na kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma husabisha mtumishi kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Mbali na hayo, ameeleza kuhusu mfumo wa ESS unafanya kazi vizuri na umewarahisishia watumishi wanaokaa mbali na makao makuu kupata huduma mbalimbali huko walipo bila kufunga safari.
Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TAGLU) wa mkoa huo, Ali Nguli amewaeleza watumushi hao kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) upo hivyo watumishi wanapopata majanga wanapokua mahala pakazi wautumie mfuko huo.
Naye Mtumishi, Patrice Sagday ameishauri serikali iliyoanzisha mfumo wa uhamisho kutekeleza kwa sababu inadaiwa kutoona walioomba kupitia mfumo huo wakihama.
Kikao kazi kimefanyika na kuwakutanisha watumishi takribani 300 kutoka katika kata za Sungwisi, Mwamala, Ndembezi, Kitangiri, Mwisi, Nkinga na Ugaka huku ikitarajia kuendelea katika Kata nyingine za wilaya hiyo.
Aidha, Mada ya Sheria na kanuni zinazoongoza utumishi wa umma, Mfumo wa ESS, Maadili ya utumishi wa umma ziliwasilishwa ikiwemo Kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Watumishi hao .
=========
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa