UTEKELEZAJI na usimamizi sahihi wa Mradi wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS) umeiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kushika nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri zote nchini.
Aidha, hatua hiyo imeiwezesha Halmashauri hiyo kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali katika Zahanati ya Mwamapuli, Matinje na Mwajinjama awamu ya kwanza huku awamu yapili ikitekeleza Dispensari ya Nguriti, Utuja, Mgazi, Itumba na Ziba.
Akizungumza katika kikao kazi kilichofanya Jumamosi Februari 08, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Sauda Mtondoo aliipogeza timu inayoongozwa na Mganga Mkuu wakiwemo wote walioshiriki katika utekelezaji wa mradi huo ambao ulipelekea kuvuna takribani sh. bilioni tatu, hivyo Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanaza kitaifa.
‘’Hongereni ! haikua kazi ndogo, ilikua kazi kubwa, hivyo mwenendo huo umetufanya kukutana leo kuweka mikakati ya kuvuna zaidi kuliko msimu uliopita kwa sababu ari tuliyonayo ya umoja tunaweza,’’ alisema Mhe. DC Sauda na kuongeza kuwa:
‘’Kila mmoja kwa nafasi yake akasimame vema hususan waliopokea fedha awamu ya kwanza kwa sababu wamebeba dhamana ya aidha kuwahi au kuchelewa kupata fedha za awamu ya pili.’’
Aliwataka Wajumbe hao kuisemea miradi hiyo kwa wananchi kwa lengo la kuhakikisha wanaifahamu kwa sababu wao ni semhemu ya usimamimizi na utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Lucas Bugota aliendelea kuipongza Idara ya Mganga Mkuu kwa kuwaheshimisha wananchi wa Igunga kufuatia Halmashauri hiyo kuongoza Kitaifa.
‘’Ninawapongeza sana, kwa kweli ni jambo kumba, Wilaya na Halmashauri ziko ngapi Tanzania nzima lakini imeonekana Igunga,’’ alipongeza Bugota.
Alieleza kuwa miradi hiyo inatekelezwa ngazi ya kijiji na Kata, hivyo Madiwani na Watendaji wa Kata ndio viongozi wakuu wasimamie fedha za serikali mpaka miradi inapokua imekamilika.
‘’Nendeni mkasimamie miradi ikamilike kwa wakati kwa sababu Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi amabazo ni za kutusaidia sisi,’’ alisema.
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Lucia Kafumu alimshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuungana na watalaamu hao katika kikao hicho kwa sababu wanaamini maneno yake ni tiba kwao na yanawapa nguvu yakwenda kuwajibika zaidi.
Naye Afisa Afya wa Wilaya hiyo, Muhoja Lubeja alisema utekelezaji wa Mradi huo unahusisha Idara ya Elimu, Afya na Maji huku kwa upande wa Afya mradi huo unajishughulisha na uhamasishaji wa vyoo ngazi ya kaya na jamii.
Alidokeza kuwa awamu ya kwanza walipokea sh. milioni 218 kati ya Sh. Milioni 727 ambazo wanatarajia kuzipokea awamu zinayofuata.
Aliweka wazi chanzo cha fedha hizo ni baada ya kufanyika uhakiki wa masuala ya afya na usafi wa mazingira ngazi ya kaya na vituo vilikidhi vigezo vilivyowekwa na wafadhili Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali.
==== //// ==== //// ==== ///// =====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa