Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inaungana na Halmashauri zote Nchi nzima kuadhimisha wiki ya chanjo ambayo hufanyika wiki ya mwisho ya mwezi April kila mwaka.
Katika wiki hii, idara ya afya itasimamia zoezi la uhamasishaji na utoaji wa chanjo za kawaida kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 ambao hawajapata kabisa chanjo au walioasi kukamilisha dozi kamili za chanjo. Pia Wilaya itakabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa surua ambao umewakumba halmashauri Jirani, kwa kuwatambua wahisiwa wote na kuwaelekeza kupata huduma sahihi ya matibabu ili kuzuia mlipuko katika halmashauri yetu.
Hadi sasa, kiwango cha uchanjaji kilichofikiwa kwa Wilaya ni asilimia 96% Tangu Mwezi Jananuari had Desemba. 2022 na kiwango cha asilimia 100% tangu Januari hadi Machi 2023 kwa chanjo ya Kifaduro, Dondakoo na Pepopunda.
Kiwango kilichofikiwa kwa chanjo ya surua ni 92% tangu Januari hadi Desemba 2022 na kiwango kilichofikiwa tangu Januari-Machi 2023 ni asilimia 100%
Pia zoezi la utambuzi wa watoto wasiochanjwa na walioasi chanjo linaendelea kufanyika ili kuhakikisha Watoto ambao wamekosa fursa ya kupata chanjo wanapata chanjo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mpango wa Taifa wa Chanjo (IVD) na Ofisi ya Rais TAMISEMI imekuwa ikiratibu zoezi la utoaji wa chanjo za UVIKO-19 nchini. Hadi kufikia mwezi Machi.2023 kiwango cha uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 ilikuwa ni 100% tangu ilipozinduliwa mwezi Agosti mwaka 2021.
Tumefanikiwa, Kuwafikia watoto wengi zaidi kwa kufanya uchanjaji wa kiwango cha 96% kwa chanjo ya Dondakoo, Kifaduro na Pepopunda na kiwango cha 92% kwa chanjo ya Surua kwa mwaka 2022.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa