Mhe Sauda Mtondoo ameshiriki Jogging pamoja na Mazoezi yalioandaliwa na Divisheni ya AFYA, Lishe na Ustawi wa Jamii ikijumuisha watumishi na wananchi wote bila kujali umriwao. Baada kumaliza mazoezi hayo Mhe; Mtondoo amewataka wananchi wote wa Wilaya ya Igunga kila mmoja popote alipo awe na tabia ya kutenga muda wa kufanya Mazoezi kwani mazoezi yanamuepusha mtu na magonjwa yasiyoambukizwa. Pia alitoa raia kwa Washiriki wote wa siku hiyo 4/3/2023,kuwa kwa wale ambao huwa wanatabia ya kufanya mazoezi wawe wanawakumbusha wanaoishi nao nyumbani kwani kukinga ni rahisi kuliko kutibu.Aidha Mhe; Mkuu wa Wilaya alitoa vyeti kwa washiriki hasa wenye umri unaoazia miaka 55 na kuendelea.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Lucia Kafumu,ametoa taarifa fupi baada ya kumaliza mazoezi uwanja wa sabasaba akiwaeleza washiriki umuhimu wa kufanya mazoezi kuwa ni pamoja na;
1 Mazoezi yanasaidia mwili kuchoma mafuta yote yaliyomo kwenye mwili yasiyohitajika.
2 Mazoezi yanafungua mishipa ya damu ili iweze kuruhusu damu itembee vizuri katika mwili.
3 Mazoezi yanasaindia sana kuimarisha ulinzi wa mwili ili mwili usipatwe na magonjwa yasioyakuambizwa
4 Mazoezi yanaimalisha uwezo wa kufikili.
5 Mazoezi yanamfanya kuwa huru,furaha,uchangamfu,kwaupifi yanaondoa msongo wa mawazo.
Alimalizia kwa kusema kuwa Divisheni (Idara) ya Afya itaweka mpango mzuri wa kuhamasisha Divisheni nyingine na Vitengo mbalimbali kuweka utaratibu mzuri wa Jogging na Mazoezi kwa kila wiki mara moja.
Aliyekuwa muwakirishi wa Mkurugenzi MUSSA ABDALAH ambaye ni Afisa UATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, amewataka Watumishi wawe na tabia ya kufanya mazoezi kama inavyoelekezwa na wataalamu wa Afya.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa