MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mhe. Sauda Mtondoo amewataka Wananchi wakiwemo wanafunzi wa shule zote za Wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele kutunza Mazingira kwa sababu wakiyatunza na yenyewe yatawatunza.
Mhe. Sauda ameto wito huo Ijumaa Januari 31, 2025 wakati wa Maadhimisho ya upandaji wa miti duniani katika Shule ya Msingi Mwayunge wilayani hapa.
Alisema Mazingira yanafaida nyingi ikiwemo kupata kimvuli, matunda na nichanzo cha mvua, hivyo wananchi wote wanatakiwa kuhakikisha wanapanda miti na kuitunza vizuri.
Pia, aliwahimiza viongozi wa vijiji, vitongoji wakiweme Madiwani kuendelea kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha kila kaya inapanda miti takribani mitano.
‘’Tukiwa na utamaduni huo hakika mji wetu wa Igunga utabadilika na kuwa kijani kwa sababu Igunga ya Kijani inawezekana,’’alisistiza.
Katika hatua nyingine, DC Sauda ametoa wito kwa wananchi wanaodaiwa kuchungia mifugo katika maeneo ambayo miti imepandwa kuacha kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu, sheria na kanuni.
“Watu wanapanda miti lakini inaliwa na mifugo kutokana na uchungaji holela, hivyo ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zinazingatiwa na kufanyiwa kazi na wale wanaochunga mifugo hovyo wadhibitiwe kwa lengo la kuhakikisha miti inayopandwa inakua na tuione Igunga ya Kijani ,’’ alisistiza DC Sauda.
Kaimu Ofisa Maliasili na Mazingira wa wilaya hiyo, Emmanuel Mnanka alisema wamefanya Kampeni mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha wanafikia lengo la kupanda miti million 1.5.
Alifafanua kuwa tangu kutokea mwezi Desema 2024 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilikwishagawa miche takribani 64,337 ya aina tofauti ikiwemo ya matunda na kimvuli.
Alieleza mbali na kugawa miti wamekuwa wakitoa elimu kwa Walimu wa Mazingira kwa lengo la kuhakikisha wanaunda vilabu vya mazingira na kuotesha vitalu vya miti.
Akizungumza katika upandaji miti huo, Diwani wa Kata ya Igunga, Athuman Mdoe alisema wamejiandaa kupanda miti mingi na kupitia sheria za Mamlaka ya Mjii wataanza kuikamata mifugo inayokula miti kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kutunza mazingira yao.
Kwa upande wa Mwalimu wa Mazingi Shule ya Msingi Mwayunge wilayani hapa, Oscar Kireboh alibainisha kuwa wanautaratibu wa kupata mbegu mbalimbali ambapo wameotesha miche 500 na wamekwishapanda miche 300 katika maeneo yao.
Naye Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule hiyo, Franck Nicholous alisema miti hiyo inawawezesha kupata kinvuli ikiwemo matunda.
Aidha, alitoa wito kwa Wachungaji wa mifugo kuhakikisha wanachungia maeneo maalumu huku wakiepuka kuchungia maeneo ambayo yamepandwa miti.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa