Mhe. Sauda Salum Mtondoo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga amewataka wawezeshaji,waheshimiwa madiwani pamoja na viongozi wote kuwa, Serikali iliagiza kutolewa elimu ya kutosha na kujenga uelewa wa pamoja kwa jamii ili kuondoa malalamiko kwa jamii,amesema jana katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Igunga
Serikali iliagiza wawezeshaji na viongozi watakao shiriki katika zoezi hili la kutambua walengwa na kuandikisha wawe walengwa wanaostahili, aliwataka kuzingatia vigezo vilivyowekwa ili kupata walengwa sahihi
“Kupitia viapo mtakavyo apa vitawaweka kwenye kitanzi,iwapo mtakiuka taratibu za utambuzi wa kaya masikini, atakae ingia kwenye mpango huu awe ni yule mwenye vigezo na vizingatiwe kusiwe na undugu wala upendeleo katika uandikishaji”alisisitiza Mhe.Mkuu wa Wilaya Igunga
Aidha aliwataka wawezeshaji watakao onekana wamekiuka taratibu katika zoezi hili la uandikishaji, wasimamizi wa zoezi hili kuwachukulia hatua stahiki
“Mapambano dhidi ya umasikini katika nchi yetu yalianza toka baada ya Uhuru takribani miaka sitini sasa na bado tunaendelea kupambana nayo utekelezaji wa shughuli za TASAF ni moja ya nyezo za kupambana na umaskini, kaya zaidi ya milioni moja zimewezeshwa na TASAF kupambana na umasikini” ameyasema hayo katika Kikao kazi Sauda Salumu Mtondoo Mhe.Mkuu wa Wilaya Igunga
Pia wale ambao hali zao za kiuchumi hazijaimalika hawataachwa bali wataendelea kupatiwa elimu ili kuondokana na umaskini, ili kuendelea kuboresha kaya zao aliongeza Mhe. Sauda Salum Mtondoo, Mkuu wa Wilaya Igunga
Amewataka viongozi walioshiriki kikao kazi hicho kuwa wanajukumu la kuendelea kuwapa msaada walengwa kwa kuendelea kuwakwamua kiuchumi kwa kuhakikisha watumishi wanaofatilia shughuli za walengwa kujiimalisha katika sekta za mifugo,kilimo na ujasiliamali ili waweze kuwaelimsha kuboresha uchumi wao
Akiongea Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji TASAF Makao Makuu Bwana Oscar Maduhu alisema kutokana na malalamiko kutoka kwenye jamii kuwa ndani ya walengwa kuna walengwa hawana vigezo au walengwa hewa ili kuwaondoa kwenye mpango hasa kaya zisizokuwa na vigezo, za viongozi, waliohama na waliofaliki zoezi hili lilifanyika katika kipindi cha mwezi wa sita 2020 na kurudiwa Disemba 2020, lengo lake lilikuwa ni kusafisha au kuhuisha daftari la walengwa au masjala ya walengwa iliyopo TASAF Makao Makuu
Kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kitatekelezwa katika halmashauri zote 184 za Tanzania bara na wilaya zote za Zanzibar kitafikia kaya 1,450,000 zenye jumla ya watu zaidi ya milioni 7,000,000 kote nchini
Mkazo mkubwa katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF umewekwa katika kuwezesha kaya zitakazo andikishwa kwenye kufanya kazi na kuongeza ili kuongeza kipato, aidha kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kitahakikisha huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa na kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na afya
Bwana Oscar Maduhu ameendelea kusema walengwa watatambuliwa na kuandikishwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, ni kaya zinazoishi katika hali duni katika vijiji, mitaa na shehia zetu.
Wanufaika ndani ya kaya ni watoto chini ya miaka 5 wanaohudhuria kliniki, wanafunzi shule za awali,shule za msingi na shule za sekondari,mama wajawazito na wana kaya wenye ulemavu ameongeza Bwana Oscar Maduhu
Aidha ameendelea kusema mpango unatoa ruzuku za aina mbili ruzuku ya msingi na ruzuku ya masharti kwa wale wanaotakiwa kwenda shule na watoto wanaohudhuria kliniki, lakini ajira za muda kwa mwanakaya mmoja aliye na uwezo wa kufanya kazi
Aliendelea kumshukuru Mkurugenzi mtendaji Wilaya kwa kutoa wataalam wengi kutoka ngazi ya kata kushiriki katika zoezi la kutambua na kuandikisha walengwa, aidha watasaini viapo vya uadilifu ambavyo vitatumika pale ambapo mwezeshaji ataandikisha kaya ambazo hazina vigezo viapo hivyo vitatumika pia kwa viongozi wa mitaa na vijiji
Amewaomba viongozi kutoa ushirikiano wataokuwepo kwenye maeneo zoezi litakapo kwenda kufanyika taarifa zitolewe mapema na viongozi watende haki na kuepuka upendeleo katika uandikishaji walengwa ili wale wanaostahili waweze kuandikishwa.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa