Familia ni chanzo cha jamii yoyote Duniani kwa kuwa kila mtu amezaliwa na amekulia katika Taasisi hii muhimu katika Jamii. Familia inaundwa na Mume,Mke na Watoto na katika utamaduni wetu Ndugu wakaribu wanakuwa sehemu ya familia.Majukumu ya Familia ni pamoja na kutoa huduma muhimu zikiwemo mahitaji ya Watoto na Familia,Ulinzi na Mawasiliano.
Kauli mbiu ya siku ya Kimataifa ya familia Duniani kwa mwaka huu 2023 ni “Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia Imara”.Kauli mbiu hii inatumika kuwakumbusha nyinyi wazazi na walezi juu ya umuhimu wa maadili mema na upendo miongoni mwa wanafamilia. Aidha inawakumbusha wanafamilia umuhimu wakuzingatia Maadili mema ya Kitanzania katika malezi na makuzi ya watoto wetu.Pia kauli mbiu hii inasisitiza upendo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayopelekea familia nyingi kusambaratika na kuacha watoto bila uangalizi wapamoja hivyo kukosa huduma muhimu.
Maadhimisho haya yanawakumbusha wazazi na walezi wajibu wenu wa msingi katika malezi ya watoto na familia hasa akina baba wajibu wenu kama wazazi au walezi kwa watoto katika maeneo makuu matatu ya msingi
Pamoja na jitihada za Serikali katika kuhimiza maadili mema na upendo katika familia zetu bado kunamatukio mengi ya ukatili wa watoto na wanawake yanayoshuhudiwa katika ngazi ya familia na katika jamii.Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na:-
Tafiti nyingi za ukatili dhidi ya watoto zinaonyesha kuwa ukatili wa watoto unafanyika zaidi nyumbani kwa asilimia 60 na shuleni kw asilimia 40 na wanaofanya ukatili zaidi ni ndugu na jamaa wa karibu na familia husika.Changamoto kubwa katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto unatokana na ukimya wa wazazi na walezi katika kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyofanyika ndani ya familia kwasababu tofautitofauti zikiwemo:-
Kuepuka hatua za kisheria dhidi ya mkosaji,mila na desturi, kuwepo kwa Imani potofu zenye madhara zinazotekelezwa katika baadhi ya familia, uelewa mdogo kuhusu malezi chanya na mawasiliano duni miongoni mwa wanafamilia.Hali hii inapelekea watoto wengi kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa katika jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa utoro shuleni ,kuongezeka kwa vitendo vya ukatili na maambukizi ya VVU.
Ili kufikia lengo la kuwa na familia imara na zenye upendo wazazi na walezi mnatakiwa kutimiza wajibu wenu kwa kuhakikisha kuwa huduma za muhimu kwa watoto wenu zinatimizwa ikiwa ni pamoja na :-
Ndugu Wananchi, Sisi sote tunatakiwa kushikamana katika kujenga familia zenye maelewano yakutosha na yenye upendo kwani ndio msingi wa uzalishaji mali utakao wawezesha kutoa huduma za msingi kwa watoto wetu na kufuatilia maendeleo yao katika makuzi, maadili na masomo yao shuleni.
Familia bora zinatakiwa kuwalea watotot wakiume na wakike kwa usawa kwani wote wanamchango ulio sawa kwa maendeleo ya Taifa.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa