Mhe: Sauda Mtondoo Mkuu wa Wilaya ya Igunga ameyataka Mashirika yasio ya Kiserikali kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia maadili na tamaduni za Kitanzania,Kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii hivyo sisi serikali tunatekeleza majukumu yetu vizuri nawasihi nanyi mkasimame imara juu ya suala la tamaduni zetu, Desturi zetu kama watanzania.Mhe; Mtondoo ameyasema hayo 15/04/2024 katika Kikao cha kuwasilisha taarifa za utekelezaji za robo za Mashirika yasio ya Kiserikali (NGOs) Wilaya ya Igunga.
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inaendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa Asasi za Kiraia na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ambao wanaratibiwa utekelezaji wa shughuli zao chini ya dawati maalum la Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) lililopo Idara ya Maendeleo ya Jamii lililoanzishwa kupitia “Mwongozo wa Majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii” mwaka 2019.
Usimamizi wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) unatekelezwa chini ya “Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 ikiwa na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 11 ya mwaka 2005 na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 na kufuatiwa na Mwongozo wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara wa mwaka
2020’’.
MASHIRIKA YANAYOTEKELEZA MIRADI YAKE KATIKA WILAYA YA IGUNGA
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina wadau wapatao 8 ambao wanatekeleza miradi yao katika sekta mbalimbali za Maendeleo hapa wilayani.
Katika idadi hiyo Mashirika sita (6) yanaendelea na utekelezaji wa miradi yao ambapo Mashirika manne (4) yanatekeleza miradi Afya, Mashirika mawili (2) yanatekeleza miradi Ngazi ya Jamii na Shirika moja (1) linatekeleza mradi wa msaada wa Kisheria.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza miradi yake hapa wilayani yamekuwa na mchango chanya katika kuchochea maendeleo kwa jamii zetu kwa kuleta/kusogeza huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazosaidia kupunguza adha na changamoto zinazozunguka jamii hizo.
MAFANIKIO
Katika usimamizi wake Halmashauri imeweza kufanikiwa ya fuatayo:-
a. Halmashauri imekuwa na Kanzidata ya Wadau wa Mashirika Iliyohuishwa.
Imefanikiwa kuzijengea uwezo Mashirika Mapya manne(4) na kuziwezesha kufanya usajili na moja limefanikiwa kusajiliwa na Wizara na kupata cheti na mengine yako katika hatua nzuri.
Kupitia ushirikiano unaotolewa na Halmashauri, Wadau wameweza kufikisha baadhi ya huduma mbalimbali ngazi ya jamii kama vile afya, elimu, msaada wa kisheria nk
Mashirika yametengeneza ajira kwa jamii kupitia shughuli zake mbalimbali.
Wadau wamepata mwitikio chanya na kuanza kutoa ushirikiano katika mambo mbalimbali mfano: Kuwwezesha Siku ya Mwanamke Duniani mwezi Machi, 2024.
Kufanyika kwa vikao vya Wadau na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kama Mwongozo wa Mashirika yasiyo ya kiserikali unavyoelekeza.
Kuimarika kwa Mahusiano baina ya Halmashauri, Wadau wa Mashirika yanayotekeleza miradi hapa wilayani na Wawakilishi wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) ngazi ya Mkoa.
MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WANAOENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI WILAYANI IGUNGA.
NA.
|
JINA LA SHIRIKA
|
MRADI
UNAOTEKELEZA |
JUMLA YA THAMANI YA MRADI |
SEKTA
|
MFADHILI
|
WANUFAIKA /WALENGWA
|
1 |
Igunga Paralegal Center (IPC)
|
Upatikanaji wa Haki Kwa Jamii
|
12,500,000.00 |
Sheria |
Legal Service
Facility - Tanzania |
Makundi Maalum
|
2 |
Management and
Development of Health (MDH) |
Afya Jumuishi
|
1,243,000,000 |
Afya |
CDC / PEPFAR
|
Makundi hatarishi
(AYGW) na Makundi Waathirika (PLHIV) |
3 |
Inland Development Tanzania (IDT)
|
ACHIEVE
|
105,592,800.00 |
Afya |
United States
Agency for International Development (USAID) |
Watoto wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI
umri wa miaka 017 |
4 |
Johns Hopkins
Program for International Education in Gynecology and Obstetrics (JHPIEGO) |
TOHARA
|
|
Afya |
United States
Agency for International Development (USAID) |
|
USAID AFYA YANGU
|
|
Afya |
United States
Agency for International Development (USAID) |
Wajawazito na watoto wachanga , Afya ya Watoto, Lishe, Chanjo, Vijana 10-24.
|
||
5 |
Elizabeth Glasser
Pediatric Aids Foundation (EGPAF) |
USAID AFYA
YANGU- NORTHERN ZONE |
78,452,656.00 |
Afya |
United States
Agency for International Development (USAID) |
Wagonjwa wa
Kifua Kikuu |
MALEZI NA MAKUZI
|
12,000,000.00 |
Ustawi wa Jamii |
Conrad Hillton Foundation
|
Watoto chini ya miaka 5
|
||
6 |
Thubutu Africa
Initiative (TAI) |
USAID AFYA YANGU
|
90,000,000.00 (kwa mwaka) |
Jamii |
USAID - JHPIEGO
|
Wanawake, Watoto na Vijana 10-24.
|
7 |
Nutrition
International (NI) |
BRIGHT
|
28,137,268,500.00
(kwa miaka saba 7) |
Lishe na
Afya ya Uzazi kwa Vijana
|
GLOBAL AFFAIRS - CANADA
|
Vijana wa Miaka 10-19 waliopo shuleni na waliopo mtaani.
|
8 |
BRAC Maendeleo
|
UWEZESHAJI WA
WASICHAN A NA WANAWAKE KIJAMII NA KIUCHUMI |
12,897,721,200.00
|
Jamii |
MASTERCARD FOUNDATION
|
|
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa