Wataalamu wa Seksheni ya Elimu Msingi,Sekondari,Ustawi wa Jamii na Kitengo Cha TEHAMA wameendesha mafunzo kwa ma Afisa Elimmu Kata, Walimu Wakuu wa shule za msingi, wakui wa shule sekondari,walimu wa takwimu wa shule za sekondari na msingi pamoja na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto mchana (Day care centers) mafunzo hayo yaliyofanyika kwa awamu nne kwa Tarafa za Igunga,Manonga,Simbo na kuhitimishwa jana tarehe 30.3.2023 katika Tarafa ya Igurubi
Akiongea katika ufungunzi wa Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Ndg, JOSEPH MAFURU, aliwataka Walimu hao kujikita kwenye misingi yao ya Uadilifu, kuzingatia sheria ya takwimu,usahihi wa takwimu,ujazaji wa takwimu kwa wakati unaotakiwa na kuuliza pale utata utakapojitokeza
‘Kwa kuwa Mafunzo yanayotolewa ni kwa ajili ya kuweka Takwimu sahihi za wanafunzi pamoja na Walimu kwani ndizo zitakazoweza kusaidia katika kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za Elimu’aliongeza Ndg, Joseph Mafuru kaimu Mkurugenzi
Aidha wakati wa mafunzo wawezeshaji walisisitiza juu ya kuijua sheria ya takwimu na umuhimu wa kuwa na takwimu Bora,kuyaelewa majedwali ya ulinganifu(consistency) na majedwali ya lazima kujazwa(compulsory items).Washiriki wa mafuzo waliweza kujua Majukumu ya walimu wa takwimu ,wakuu wa shule na ma Afisa elimu kata,katika ngazi zao za kiutendaji
Nao washiriki wameishumuru serikali kubuni mpango huu wa mafunzo kwa walimu kwani imewapa uelewa mkubwa katika kutumia mifumo, pia walitoa mapendekezo ya namna ya kufanyia maboresho mfumo wa wa sensaelimu msingi kuweza kuruhusu mtumiaji kufanya kazi akiwa eneo lisilo la mtandao yaani (offline )ili kazi isikwame kwa kuzingatia maeneo yaliyo mengi hayana mtandao.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa