MKUU wa Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora, Mhe. Sauda Mtondoo amesema atachukua hatua dhidi ya hujuma ya kuweka uchafu, mchanga laini, maji au vikonyo katika zao la Pamba unaofanywa na baadhi ya watu.
DC. Sauda ametoa ahadi hiyo Al hamisi mwezi Aprili 17, 2025, baada ya kutembelea Viwanda vya Manispaa ya Shinyanga akiwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Napinduzi (CCM) na Halmashauri.
Alisema msimu huu watahakikisha wanakua makini kuwasimamia viongozi wa AMCOS kwa lengo la kuhakikisha Pamba inakusanywa katika ubora unaotakiwa.
‘’Watu watakaojaribu kufanya uharibifu wa aina yoyote ni lazima tuchukue hatua stahiki na kali kwa lengo la kuhakikisha inakua fundisho kwa wengine wasijaribu kufanya hivyo kwa sababu ya kuendelea kulinda ubora wa Pamba inazalishwa Igunga,’’ alisema Mhe. DC. Sauda.
Aidha, aliahidi kukomesha uharibifu na uchafuzi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa AMCOS katika maeneo ya ukusanyaji wa zao hilo.
Alieleza tabia hiyo isiyokua ya kiadilifu sio tu inazitia hasara Kampuni lakini pia serikali, hivyo nilazima wasimame kidete kwa kubanana kwa lengo la kuhakikisha msimu utakapoanza yasirudie yaliojitikeza katika msimu uliopita.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Igunga, Mafunda Temanya alisema wataendelea kutekeleza Ilani ya Chama ikiwemo kuwalinda wakulima wa Pamba.
‘’Ndani ya AMCOS kuna viongozi sio waaminifu ndio maana wanataka kuwachafua wakulima wakati wako vizuri, hivyo wanachafuliwa na Watu wajanja wajanja,’’ alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Lucas Bugota alisema mpango wa kuzalisha Pamba umeipandisha Halmashauri hiyo kwa sababu inapata mapato ya kutosha, hivyo changamoto hiyo wameiona na kuahidi kuifanyia kazi kwa kuwasimamia wanaopokea Pamba.
Kwa Upande wa Mmiliki wa Kampuni ya Gaki Investment, Gasper Kileo alisema Mkulima anafikisha Pamba safi na inachafuliwa kwenye Ghala la kuhifadhia, hivyo aliomba Makatibu Meneja wapewe semina elekezi kwa sababu hakuna Mkulima anayekubali kuchafua mbegu au Pamba.
Alidokeza wanapata hasara ya moja kwa moja kwa sababu michanga inayokutwa kenye pamaba inaua mitambo ya uchakataji, hivyo wanaviomba Vyombo kuwa vikali dhidi ya watu wanaochanganya maji na mchanga kwenye Pamba.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Fresho Investment, Salman Arab alisema msimu uliopita walipata hasara ya jumla sh. Milioni 650 zilizotokana na uchafu kwenye Pamba.
==== //// ==== //// ==== //// ====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa