Mheshimiwa George Joseph Kakunda Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa OR-Tamisemi, akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za miradi ya maendeleo Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora amewataka watumishi kuilezea Serikali vizuri kwa wananchi juu ya kazi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya awamu ya tano kuwa ni mzalendo wa kweli anayelipenda Taifa la Tanzania hivi karibuni.
Mhe.Naibu Waziri OR-Tamisemi aliwaasa watendaji wa Serikali,watendaji wa kata na vijiji, wakuu wa shule na Walimu wakuu wote kueleza maswala mazuri yote yanayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano. Pia aliendelea kusema watumishi ndio wajuzi wa mambo yote mazuri yanayofanywa na Serikali kwani mambo yote yanafikia Halmashuri mwananchi wa kawaida hajui ugumu wa fedha anachotaka kuona ni huduma nzuri ya maji, mtoto asome na kupata matibabu,si jukumu la Watumishi wa Serikali si kukaa Bar na kuisema Serikali kuwa ni mbaya.
“Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la madaraka ya Rais, ameteua watumishi kutekeleza baadhi ya majukumu kwa niaba yake watumishi ndio wenye jukumu la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano kutekeleza majukumu yake” alisema Mhe.Naibu Waziri OR-Tamisemi.
Mhe. Naibu Waziri OR-Tamisemi aliwaasa watumisha kufanya kazi kwa weledi kwa kufata kanuni,taratibu na sharia za nchi na kuwataka Wakurugenzzi na Wakuu wa Idara kufanya kazi kwa ushirikiano na sio kuleta misuguano katika maeneo ya kazi kwani inakwamisha maendeleo kwa wananchi.
Aliendelea kusema tangu mwaka 1994 kuna kampuni moja ilikuwa inalipwa kila mwezi karibu bilioni saba na kununuliwa mafuta, Watanzania kupitia pesa hizo wameumia vya kutosha hivyo Mhe.Rais ameamua kuzalisha umeme wa kutosha kule Morogoro ambapo utazalishwa umeme wa megawatt 2100 ili kukuza uchumi wa viwanda.
Nae Mhe. John Gabriel Mwaipopo Mkuu wa Wilaya ya Igunga ikisoma taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya maji na Shule kwa Mgeni Rasmi Mhe. Naibu Waziri OR-Tamisemi alisema Mhe. Mgeni Rasmi Wilaya ya Igunga imepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za sekondari kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo katika awamu mbili hadi sasa. Awamu ya kwanza tumepokea jumla ya Tshs. 316,000,000.00 zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu ya shule mbili za Nanga na Ziba Sekondari, katika fedha hizo Nanga Sekondari ilipokea Tshs. 241,000,000.00 mnamo tarehe 05/07/2017 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni mawili (2) kwa Tshs. 150,000,000.00, vyumba vya madarasa vinne (4) kwa Tshs. 80,000,000.00 na matundu ya vyoo kumi (10) kwa Tshs. 11,000,000.00. Ziba Sekondari ilipokea Tshs. 75,000,000.00 mnamo tarehe 12/09/2017 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja (1)
Katika awamu ya pili Wilaya ya Igunga imepokea tshs. 190,000,000.00 mnamo tarahe 29/12/2017 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Ziba kwa mchanganuo ufuatao; Ujenzi wa mabweni mawili (2) kwa Tshs. 150,000,000.00, na ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili 2 kwa Tshs. 40,000,000.00.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa