Mhe. Sauda Salum Mtondoo, Mkuu wa Wilaya ya Igunga amewakumbusha Watendaji wa Kata Saba waliokabidhiwa Pikipiki zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi jana tarehe 28.02.2023 katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
Mh. Mkuu wa wilaya alianza kushukuru Wizara OR Tamisemi kwa kuliona kutatua changamotoza usafiri kwa wasimamizi wa Kata, Hivyo Halmashauri inapaswa kutenga kwenye Bajeti yake ya mapato ya ndani ili kuweza kununua pikipiki tno kila Mwaka kwa kusaidia kata kumi na tisa ambazo hazijapata usifiri
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Igunag Bw.Joseph Elias Sambo, alimweleza Mgeni rasmi kuwa Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya Kata 35 kati ya hizo kata kumi na tisa (19) hazijaweza kuwezeshwa kupata vitendea kazi
“Pikipiki zilizogawiwa kwenu leo mgao wake umezingatia vipaumbele hasa katika swala la Mapato,umbali, changamoto zinazokabili kata husika ikiwemo swala zima la migogoro hivyo menejementi imeliona hilo, hivyo waliopata pikipiki hizo wajitahidi kuvitunza” alisisitiza Mhe.Mkuu wa Wilaya Igunga
Aliendelea kusema pikipiki hizi ni kwa ajili ya kusimamia mapato jitahidini kuhahikisha mnaenda kusimamia uongezaji wa mapato ili kuweza kusaidia wengine kuweza kupata vitendea kazi kwa bajeti ya mapato ya ndani ya Halmashauri
Aidha alimtaka Afisa mipango wa halmashauri kushirikiana na Menejimenti kufanya jitihada za makusudi katika upangaji wa Bajeti ili Kata nyingine ambazo hazijapata vitendea kazi ziweze kupata kwa kununuliwa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani
Akiongea Afisa Mtendaji Kata ya Isakamaliwa Bw.Misambo Kanyelele ambaye alishukuru kwa niaba ya watendaji wezake hao saba (7) alisema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Hassan Suluhu kwa kuwajali kwani miaka yote aliyofanya kazi hakuwahi kupata chombo cha usafiri Pamoja na Ofisi ya Rais tamisemi kwa kuwajali watumishi wa kada za chini
Mhe. Sauda Salum Mtondoo, Mkuu wa Wilaya ya Igunga amewataka viongozi wa halmashauri na menejimenti kuendelea kutoa ushirikiano katika kudumisha misingi ya kazi kwa kufata sheria, taratibu na kanununi za kiutumishi katika maeneo yao ya kiutawala.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa