Kamati ya Maafa Wilaya ya Igunga imekaa na kubainiasha Athari zinazoweza kujitokeza kutokana na Mvua za Elnino zinazotajiwa Msimu wa Mwaka 2023/2023,Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga 9/11/2023,kikiongozwa na Mwenyekiti wa Maafa ambaye ni Mhe;Sauda Mtondoo Mkuu wa Wilaya ya Igunga.Athari zilibainishwa na kuweka Mikakati ya kukabiliana na Athari hizo kama zinavyoonekana katika Jedwari hapo chini.
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA MVUA ZA ELNINO ZINAZOTARAJIWA MSIMU HUU WA 2023/2024.
NA:
|
ATHARI ZINAZOTARAJIWA
|
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATAARI
|
1 | Mafuriko kutokana na mvua nyingi
|
|
2 | Kuharibika kwa miundombinu ya barabara, madaraja, umeme na maji
|
|
3 | Kusimama au kupungua kasi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya barabara na kupelekea kutofikishwa kwa mahitaji ya ujenzi
|
|
4 | Ongezeko la utoro kwa wanafunzi kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya barabara kuelekea shuleni
|
|
5 | Kuharibika kwa makazi mfano kubomoka kwa nyumba kunakoweza kusababishwa na maji yaliyotuama kwa muda mrefu katika makazi na kuezuliwa kwa majengo kunakoweza kusababishwa na pepo kali zinazoweza kuambatana na mvua nyingi.
|
|
6 | Kuharibika kwa mashambaa kutokana na mmomonyoko wa ardhi unaoweza kusababishwa na mafuriko.
|
|
7 | Upungufu wa chakula unaoweza kutokea kutokana na mazao kusombwa na mafuriko au mazao hayo kutofanya vizuri kwa maji kutuama kwa muda mrefu shambani.
|
|
8 | Ongezeko la mlipuko wa magonjwa mfano kipindupindu, kuhara, malaria na homa ya matumbo
|
|
9 | Mlundikano wa taka kutokana na taka hizo kusombwa na maji toka maeneo mengine
|
|
10 | Kupungua kwa upatikanaji wa maiji safi na salama kutokana na vyanzo vya maji kuchafuliwa na tope linalotokana na mafuriko
|
|
11 | Kuongezeka kwa gharama za kusafisha maji kutokana na maji kuchafuliwa na tope.
|
|
12 | Kung’oka na kuanguka kwa miti kutokana na mmomonyoko wa udongo Upepo mkali unaoweza kuambatana na mvua kubwa.
|
|
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa