• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA AELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU YA Mhe: RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Tarehe iliyowekwa: July 1st, 2024


Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 6,912. Kati ya hizo kilometa za mraba 1,123 ni za misitu na kilometa  za mraba 3,145 zinafaa kwa kilimo. Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi  ya mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina jumla ya watu  546,204 (wanaume 266,554 na wanawake 279,560) na inaundwa na

Tarafa 4, Kata 35, Vijiji 119 na Vitongoji 754.

Hali ya Uchumi na Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inategemea zaidi Sekta ya Kilimo ambayo inachangia zaidi ya asilimi 50 ya pato la Wilaya na wananchi. Aidha, mapato ya ufugaji, uvuvi, na shughuli za viwandani ni ajira mbadala zinazochangia katika pato la Wilaya na wakazi wake.

Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu  ya sita, Halmashauri ya wilaya ya Igunga imepokea jumla ya Tshs.26,417,666,725.24 ambazo zimeweza kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kupitia fedha hizo za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imeweza kupata mafanikio mengi kupitia sekta mbalimbali.

SEKTA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

IDADI YA SHULE ZA MSINGI.

 

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kabla ya serikali ya awamu ya sita  ilikuwa na jumla ya shule za msingi 138 lakini hadi sasa ina jumla ya shule

148 za msingi.Ongezeko hili ni kutokana na fedha ambazo Serikali ya awamu ya sita imeweza kutupatia ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 tumeweza kujenga shule mpya mbili za msingi ambazo zipo katika kiwango bora na wanafunzi wameanza kusoma katika shule hizo.Tumeweza kuwahamisha wanafunzi kutoka kwenye shule zilizokuwa na mrudikano na kuwapunguzia umbali.




Jedwali: Idadi ya Shule za Msingi.

Mwaka
Serikali
Binafsi
Jumla
2021
131
7
138
2022
132
7
139
2023
141
7
148
2024
141
7
148

 

VYUMBA VYA MADARASA.

Kabla ya serikali ya awamu ya sita Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ilikuwa na vyumba vya madarasa 980, sasa kunavyumba vya madarasa 1,083.Hii ni hatua kubwa ambayo imefanyika chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

IDADI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ilikuwa na walimu 1,283 na kwa sasa hivi walimu waliopo ni 1,324 wa msingi.Uwajibikaji wa Walimu hawa umechangia kwa kiwango kikubwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kutoka asilimia 64.28 na kufikia asilimia 77.74

ELIMU SEKONDARI:

IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI

Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita,idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka shule 34 (30 za serikali na 4 za watu binafsi) hadi shule 44 (39 za serikali na tano (5) za watu binafsi.Aidha idadi ya wanafunzi katika shule za serikali imeongezeka kutoka wanafunzi 11,052 mwaka 2021 hadi wanafunzi 13,794 mwaka 2024.

      

 Jedwali:Idadi ya shule za sekondari

Na
Mwaka
Idadi ya Shule
Idadi ya wanafunzi
Serikali
Binafsi
Serikali
Binafsi
1
2021
30
4
11,052
2,456
2
2022
36
4
12,468
2,906
3
2023
39
5
13,794
3,068
4
2024
39
5
13,794
3,068




VYUMBA VYA MADARASA.

Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita idadi ya vyumba vya madarasa imeongezeka kutoka vyumba 335 hadi sasa kunavyumba 498 vya madarasa ambayo ni ongezeko la vyumba 133 katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita.

IDADI YA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

Halmashauri ya wilaya ya Igunga ilikuwa na walimu 362 wa Sekondari na kwa sasa idadi ya walimu imeongezeka na kufikia jumla ya walimu 495 wa sekondari. Uwajibikaji wa walimu hawa umechangia kwa kiwango kikubwa cha ufaulu kwa kidato cha pili kutoka 88% hadi 91%,kwa upande wa kidato cha nne ufaulu umeongezeka kutoka 95% hadi 99% na kidato cha sita ufaulu umeendelea kuwa wa 100% katika kipindi chote cha serikali ya awamu ya sita.

Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita, idadi ya shule zilizokuwa zinatoa huduma ya Hosteli za wanafunzi imeongezeka kutoka shule 10 hadi shule 17. Upatikanaji wa Hosteli hizi zimeweza kuwapunguzia wanafunzi waliokuwa wanatoka maeneo ya mbali, kupunguza utoro wa rejereja na kuongeza ufaulu.

SEKTA YA AFYA

HALI YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA AFYA NA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Hali ya miundombinu ya afya na upatikanaji wa huduma za afya kabla ya awamu ya Sita(6) tulikuwa na vituo vya afya 4 na kwa sasa vituo vya afya vimeongezeka na kufikia 6. Aidha kwa upande wa Zahanati tulikuwa na Zahanati 53 kwa sasa zimeongezeka na kufikia zahanati 64.Hii  ni kutokana na jitihada kubwa ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuhakikisha kwamba wananchi wanasogezewa huduma karibu hasa huduma za afya.

Hospitali ya Wilaya kabla ya Awamu ya Sita (6) haikuwa na jengo la wagonjwa mahututi lakini chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania ilitupatia fedha Tsh 383,022,684.00 kwa ajili ya jengo la wagonjwa mahututi (ICU) ambalo kwa sasa limekamilika na huduma inatolewa.




Aidha kwa kipindi cha serikali ya awamu ya sita jumla ya Tsh 3,170,819,130.00 zimetumika kwa ajili ya kununua dawa katika Bohari ya dawa (MSD) ambayo ni Ruzuku (Receipt in Kind). Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa ni 90%. Kwa sasa tunaendelea na ujenzi wa majengo manne (4) ambayo ni OPD, Wodi ya Wanaume, Jengo la kuhifadhia maiti na jengo la Mionzi kwa gharama ya Tsh. 900,000,000/=

 

HUDUMA YA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

Idadi ya vifo vya akina mama vitokanavyo na matatizo ya uzazi imepungua kutoka 92/100,000 mwaka 2020 hadi 57/100,000 kwa mwaka 2023.Idadi ya vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 15/1000 mwaka 2020 hadi 4/1000 mwaka 2023.Idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) imepungua kutoka 113/1000 mwaka 2020 hadi 6/1000 mwaka 2023. Mafanikio yote haya yamechangiwa na uboreshaji mkubwa wa huduma za Afya ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

SEKTA YA KILIMO, UFUGAJI NA UVUVI

Kwa upande wa Maafisa Ugani wa kilimo ilikuwa 52 sasa hivi tuna maafisa Ugani 50. Hata hivyo tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita kwa kutupatia vifaa kwa ajili ya shughuli za kilimo hasa Pikipiki ambapo kwa kipindi hicho tulikuwa na pikipiki 37 na sasa hivi tuna Pikipiki 49 ambapo Maafisa Ugani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wanapikipiki hii inapelekea kuwa na uwezo wa kuwafikia wakulima 10 hadi 15 kwa siku hii imeongeza tija katika shughuli za kilimo na uzalishaji wa mazao.

Yapo mengi ambayo yametekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya  Igunga katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wetu na wananchi wa Igunga wanashuhudia maendeleo makubwa.

Kwa niaba ya wananchi nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mhe.DKT.Samia Suluhu Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa utekelezaji wa kishindo wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).




Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa