Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 6,912. Kati ya hizo kilometa za mraba 1,123 ni za misitu na kilometa za mraba 3,145 zinafaa kwa kilimo. Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina jumla ya watu 546,204 (wanaume 266,554 na wanawake 279,560) na inaundwa na
Tarafa 4, Kata 35, Vijiji 119 na Vitongoji 754.
Hali ya Uchumi na Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inategemea zaidi Sekta ya Kilimo ambayo inachangia zaidi ya asilimi 50 ya pato la Wilaya na wananchi. Aidha, mapato ya ufugaji, uvuvi, na shughuli za viwandani ni ajira mbadala zinazochangia katika pato la Wilaya na wakazi wake.
Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita, Halmashauri ya wilaya ya Igunga imepokea jumla ya Tshs.26,417,666,725.24 ambazo zimeweza kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kupitia fedha hizo za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imeweza kupata mafanikio mengi kupitia sekta mbalimbali.
SEKTA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI
IDADI YA SHULE ZA MSINGI.
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kabla ya serikali ya awamu ya sita ilikuwa na jumla ya shule za msingi 138 lakini hadi sasa ina jumla ya shule
148 za msingi.Ongezeko hili ni kutokana na fedha ambazo Serikali ya awamu ya sita imeweza kutupatia ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 tumeweza kujenga shule mpya mbili za msingi ambazo zipo katika kiwango bora na wanafunzi wameanza kusoma katika shule hizo.Tumeweza kuwahamisha wanafunzi kutoka kwenye shule zilizokuwa na mrudikano na kuwapunguzia umbali.
Jedwali: Idadi ya Shule za Msingi.
Mwaka
|
Serikali
|
Binafsi
|
Jumla
|
2021
|
131
|
7
|
138
|
2022
|
132
|
7
|
139
|
2023
|
141
|
7
|
148
|
2024
|
141
|
7
|
148
|
VYUMBA VYA MADARASA.
Kabla ya serikali ya awamu ya sita Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ilikuwa na vyumba vya madarasa 980, sasa kunavyumba vya madarasa 1,083.Hii ni hatua kubwa ambayo imefanyika chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
IDADI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ilikuwa na walimu 1,283 na kwa sasa hivi walimu waliopo ni 1,324 wa msingi.Uwajibikaji wa Walimu hawa umechangia kwa kiwango kikubwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kutoka asilimia 64.28 na kufikia asilimia 77.74
ELIMU SEKONDARI:
IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita,idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka shule 34 (30 za serikali na 4 za watu binafsi) hadi shule 44 (39 za serikali na tano (5) za watu binafsi.Aidha idadi ya wanafunzi katika shule za serikali imeongezeka kutoka wanafunzi 11,052 mwaka 2021 hadi wanafunzi 13,794 mwaka 2024.
Jedwali:Idadi ya shule za sekondari
Na
|
Mwaka
|
Idadi ya Shule
|
Idadi ya wanafunzi
|
||
Serikali
|
Binafsi
|
Serikali
|
Binafsi
|
||
1
|
2021
|
30
|
4
|
11,052
|
2,456
|
2
|
2022
|
36
|
4
|
12,468
|
2,906
|
3
|
2023
|
39
|
5
|
13,794
|
3,068
|
4
|
2024
|
39
|
5
|
13,794
|
3,068
|
VYUMBA VYA MADARASA.
Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita idadi ya vyumba vya madarasa imeongezeka kutoka vyumba 335 hadi sasa kunavyumba 498 vya madarasa ambayo ni ongezeko la vyumba 133 katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita.
IDADI YA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI
Halmashauri ya wilaya ya Igunga ilikuwa na walimu 362 wa Sekondari na kwa sasa idadi ya walimu imeongezeka na kufikia jumla ya walimu 495 wa sekondari. Uwajibikaji wa walimu hawa umechangia kwa kiwango kikubwa cha ufaulu kwa kidato cha pili kutoka 88% hadi 91%,kwa upande wa kidato cha nne ufaulu umeongezeka kutoka 95% hadi 99% na kidato cha sita ufaulu umeendelea kuwa wa 100% katika kipindi chote cha serikali ya awamu ya sita.
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita, idadi ya shule zilizokuwa zinatoa huduma ya Hosteli za wanafunzi imeongezeka kutoka shule 10 hadi shule 17. Upatikanaji wa Hosteli hizi zimeweza kuwapunguzia wanafunzi waliokuwa wanatoka maeneo ya mbali, kupunguza utoro wa rejereja na kuongeza ufaulu.
SEKTA YA AFYA
HALI YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA AFYA NA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Hali ya miundombinu ya afya na upatikanaji wa huduma za afya kabla ya awamu ya Sita(6) tulikuwa na vituo vya afya 4 na kwa sasa vituo vya afya vimeongezeka na kufikia 6. Aidha kwa upande wa Zahanati tulikuwa na Zahanati 53 kwa sasa zimeongezeka na kufikia zahanati 64.Hii ni kutokana na jitihada kubwa ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kwamba wananchi wanasogezewa huduma karibu hasa huduma za afya.
Hospitali ya Wilaya kabla ya Awamu ya Sita (6) haikuwa na jengo la wagonjwa mahututi lakini chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitupatia fedha Tsh 383,022,684.00 kwa ajili ya jengo la wagonjwa mahututi (ICU) ambalo kwa sasa limekamilika na huduma inatolewa.
Aidha kwa kipindi cha serikali ya awamu ya sita jumla ya Tsh 3,170,819,130.00 zimetumika kwa ajili ya kununua dawa katika Bohari ya dawa (MSD) ambayo ni Ruzuku (Receipt in Kind). Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa ni 90%. Kwa sasa tunaendelea na ujenzi wa majengo manne (4) ambayo ni OPD, Wodi ya Wanaume, Jengo la kuhifadhia maiti na jengo la Mionzi kwa gharama ya Tsh. 900,000,000/=
HUDUMA YA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO
Idadi ya vifo vya akina mama vitokanavyo na matatizo ya uzazi imepungua kutoka 92/100,000 mwaka 2020 hadi 57/100,000 kwa mwaka 2023.Idadi ya vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 15/1000 mwaka 2020 hadi 4/1000 mwaka 2023.Idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) imepungua kutoka 113/1000 mwaka 2020 hadi 6/1000 mwaka 2023. Mafanikio yote haya yamechangiwa na uboreshaji mkubwa wa huduma za Afya ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.
SEKTA YA KILIMO, UFUGAJI NA UVUVI
Kwa upande wa Maafisa Ugani wa kilimo ilikuwa 52 sasa hivi tuna maafisa Ugani 50. Hata hivyo tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita kwa kutupatia vifaa kwa ajili ya shughuli za kilimo hasa Pikipiki ambapo kwa kipindi hicho tulikuwa na pikipiki 37 na sasa hivi tuna Pikipiki 49 ambapo Maafisa Ugani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga wanapikipiki hii inapelekea kuwa na uwezo wa kuwafikia wakulima 10 hadi 15 kwa siku hii imeongeza tija katika shughuli za kilimo na uzalishaji wa mazao.
Yapo mengi ambayo yametekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wetu na wananchi wa Igunga wanashuhudia maendeleo makubwa.
Kwa niaba ya wananchi nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mhe.DKT.Samia Suluhu Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa utekelezaji wa kishindo wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa