Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga Bi Fatuma O. Latu akiwa na Kamati ya Fedha na Mipango wamefanya ziara ya kukagua vyanzo vya Mapato vya Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Na kujionea Shughuli mbali mbali za uvuvi zinazofanyika katika mialo ya Maturubaini na Mhama mmoja kata ya Itumba na Lugubu wanakopatikana kwa wingi samaki aina ya Kambale na Kamongo.
Aidha Mkurugenzi mtendaji ametoa wito kwa makampuni na mashirika pamoja na watu binafsi kuja kuwekeza wilayani Igunga katika Kutumia fursa ya Uvuvi kwenye bonde La Wembere.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa