Mkuu wa wilaya ya IGUNGA, mh. Sauda Salum Mtondoo Leo Oktoba 26 ametembelea katika kata ya Mwamashiga na kusikiliza kero za wananchi.
Akiwa katika vijiji vya Bulenya na Mwamashiga katani hapo amewaasa wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi hususani kuelekea mwanzo wa mvua za masika.
Pia amewatangazia fursa wananchi ya kupata mafunzo ya ujasiriamali bure yatakayo tolewa na mjasiriamali mbobezi Bi.MariaSamwel Isdory, ambapo watajifunza kutengeneza Sabuni za miche na za maji ,Batiki, vikapu na vingine vingi jambo litakalo wasaidia kuongeza kipato katika familia zao badala ya kutegemea kilimo kama chanzo pekee cha kipato.
Aidha katika kuelekea mwaka mpya wa masomo2024/2025 amewataka wazazi kuwaandikisha elimu ya awali watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka minne huku wale wenye umri wa kuanzia miaka saba waandikishwe darasa la kwanza.
Katika hatua nyingine amewakumbusha wakulima wa zao la pamba kuhakikisha Wanasafisha mashamba yao kwa kuchoma moto masalia ya miti ya pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.
Ameeleza kua kitalu cha kuzalisha mbegu za pamba kipo katika wilaya hii hivyo wasiichezee fursa hiyo muhimu na kuongeza ufanisi ili kuendelea kua na vigezo vya kitalu hicho kusalia hapa kisipelekwe sehemu nyingine.
Mwisho amewahakikishia serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Daktari Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza ilani ya chama kwa kuendelea kutenga fedha nyingi za maendeleo katika maeneo ya Igunga hivyo hawana budi kuiunga mkono serikali.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa