MSIMAMIZI wa Uchaguzi 2025 ngazi ya Majinbo ya Igunga na Manonga, Hamisi Hamisi amemkabidhi fomu ya kugombea ubunge mgombea wa jimbo la Manonga kwa chama cha N.R.A. Mhe. Lwatakubi Sospeter Kabungulu.
Ndug. Hamisi amekabidhi fomu hiyo leo Al hamisi Agosti 14, 2025 katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo hayo wilayani Igunga mkoani Tabora.
Aidha, zoezi la kuchukua fomu za uteuzi limeanza na linatarajiwa kutamatika ifikapo Agosti 27 mwaka huu.
======= /////// ======
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa