• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA DED WATOA ZAWAZI KWA WASIMAMIZI WA MIRADI KWA UKAMILIFU

Tarehe iliyowekwa: January 31st, 2026

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mhe. Shabani Hemed amempongeza Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiletea Igunga fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo.


Aidha, ametoa zawadi kwa Mkuu wa shule ya sekondari Mwisi,  Baraka Magoma na Mganga Mfawidhi kituo cha afya Ziba, Kassim Hashim huku Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari,  Seleka Mtobi na Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe,  Lucia Kafumu wakipongezwa kwa kuwasimamia  kikamilifu watumishi hao waliosimamia vema miradi ya maendeleo.


Mhe. Hemed ametoa pongezi na zawadi hizo leo, Ijuamaa Januari 30, 2026 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri mjini Igunga.


Amesema Dk. Samia ameleta hizi fedha kwa kutupendelea sisi wanaigunga ziwaletee wananchi maendeleo, hivyo amewataka wasimamizi kuwa na tabia ya kutembelea miradi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.


"Sisi sote ni viongozi na tunaowajibu wa kujua kila kitu kinachoendelea na kuwaeleza wananchi kwamba Dk. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha zilizofanya kadha wa kadhaa," amesisitiza.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Sauda Mtondoo amesema serikali inafanya kazi kubwa ya kutafuta fedha na kuleta kutekeleza miradi mbalimbali, hivyo tuisimamie na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora.


Aidha, amewasisitiza kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa lengo la kufikia malengo ya kupanda miti 1.5 milioni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


Pia, amewakumbusha viongozi hao kuwaelimisha wananchi kutumia vyoo na kufuata kanuni za afya kwa lengo la kuepukana na magonjwa ya mripuko.


Katika hatua nyingine, amewahimiza kuwakumbusha wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule kwa lengo la kupata tija kupitia miundombinu mbalimbali iliyojengwa na serikali.


"Sisi viongozi tuliopewa dhamana tuwe mstari wa mbelee kutii maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na serikali na wananchi watafuata mlengo huo," amesema.


Akizungumza katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Selwa Hamid amemshukuru Rais Dk. Samia kwa mema aliyowafanyia ikiwemo ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi Mkuu.


Amesema Halmashauri hiyo imepangiwa kukusanya sh. 6.9 bilioni, hivyo wanayo kazi kubwa kuhakikisha wanafikia asilimia 100 ya ukusanyaji.


Aidha, kwa upande wa miradi amesema wanamshukuru Rais Dk. Samia ambaye aliiletaa Halmashauri  hiyo zaidi ya sh. 16 bilioni kutekeleza miundombinu mbalimbali katika majimbo ya wilaya hiyo.

============////////////////////////////////////


Matangazo

  • WAHI FURSA ZA UWEKEZAJI IGUNGA September 25, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA October 28, 2025
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA DED WATOA ZAWAZI KWA WASIMAMIZI WA MIRADI KWA UKAMILIFU

    January 31, 2026
  • IGUNGA MATUMIZI YA KIDIJITALI YASHIKA KASI

    January 29, 2026
  • MAFUNZO YAWAONGEZEA UJUZI NA UMAKINI MADIWANI NA WATAALAMU KUIONGOZA HALMASHAURI

    January 24, 2026
  • MWENYEKITI MTEULE ATOA DIRA KUIONGZA HALMASHURI KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

    December 05, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa