• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

RUZUKU ALIYOITOA RAIS DK. SAMIA KWENYE KILIMO YAWANUFAISHA WAKULIMA ZAO LA PAMBA IGUNGA

Tarehe iliyowekwa: March 15th, 2025

Na HEMEDI MUNGA

Pamba! Dhahabu Nyeupe. Hivyo ndivyo wanavyoamini wakulima na viongozi wanaosimamia zao hilo Wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora kutokana na mafanikio lukuki ambayo Halmashauri hiyo imeyapata.

Pamba ni nyuzi asilia inayotokana na nyuzi laini za mbegu ya mmea wa pamba ambayo ni moja ya nyuzi za asili zinazotumiwa duniani na kujulikana kwa faraja na uimara wake.

Aidha, hupandwa katika hali ya hewa ya joto ambapo nyuzi zake zinavunwa na kusindikwa kwa lengo la kuunda aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo nguo, mafuta na nyuzi za vitambaa.

Mbali na wilaya ya Igunga mikoa mingine inayolima zao hilo ni Simiyu, Mara, Shinyanga, Singida, Tabora, Katavi, Kagera, Kigoma, Manyara, Dodoma, Morogoro, Tanga, Iringa, Kilimanjaro na Pwani.

Kwa mujibu wa tafiti anuai zinaeleza takrabani asilimia 40 ya watanzania wananufaika na zao la pamba katika mnyororo wa thamani kuanzia uzalishaji, ununuzi, uchambuaji, usafirishaji, mauzo ya nje ya nchi na uzalishaji wa nguo hapa nchini.

Katika kuthibisha hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga katika mwaka wa fedha 2024 hadi 2025 ilikisia kukusanya ushuru wa zao la pamba sh. 792.0 milioni ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2025 ilikusanya sh. 995.704 milioni sawa na asilimia 126 huku ikikusudia kukusanya sh. 1.050 bilioni mwaka wa fedha ujao.

Makisio hayo yanatokana na kuwepo kwa pamba nyingi msimu huu inayosadikika kupatikana kutokana na uwekezaji mkubwa wa pembejeo uliofanywa na serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Bodi ya Pamba.

Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii, Ofisa Mkaguzi wa Bodi ya Pamba wa Wilaya hii, Benjamin Madama amesema  serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia kupitia Bodi hiyo ilitekeleza mikakati ya kuongeza tija na uzalishaji wa Pamba ikiwemo kusimamia usafi na ubora wa Pamba inayozalishwa kwa lengo la kuongeza thamani katika zao hilo.

Amedokeza mikakati hiyo ilizingatia Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Bodi ya Pamba, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo.

Ameweka wazi Bodi hiyo ilisambaza pembejeo ikiwemo mbegu kilogramu 1,970,000, viuadudu eka paki 1,050,000 na vinyunyuzi bomba 8,500 ambapo ilihakikisha wakulima wote wanapata kulingana na mahitaji yao.

Ameongeza Bodi hiyo ilileta Matrekta Manne ya kulimia, Matrekta mawili na Drone tano za kupulizia dawa kwa lengo la kurahisisha zoezi hilo na kufanikiwa kupulizia ekari 20,000.

Mbali na hayo,  alisema serikali iliajiri Maofisa Kilimo 52 na kuwapatia Wakulima Wawezeshaji 160 mafunzo na usafiri wa baiskeli  kwa lengo la kushirikiana na Wagani wa serikali na wa Mradi wa Jenga Kesho Bora (BBT) kuongeza nguvu ya kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba kwa wakulima.

Sewa Hamid Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hii, amemshukuru Rais Dk. Samia kuwaletea trekta na kiwanda cha kuchakata mbegu kwa lengo la kuongeza tija kwenye zao la pamba.

 ‘’Tuweke dhamira ya kweli msimu huu kwa kuanza mimi na wewe ukiletewa pamba chafu mrudishie aliyekuletea na kumwambia kuwa pamba hiyo haitakubalika, hivyo ukimrudisha mkulima mmoja tu salamu zitafika kwa wakulima wote,’’ amesema.

Amethibisha kuwa msimu huu kutokana na uwekezaji wa serikali pamba ipo nyingi, nyeupe, nzuri na yenyekuvutia, hivyo amevitaka vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) wakiwemo wakulima kujiepusha kuweka mawe, mchanga na maji kwenye pamba.

Kauli hiyo inakuja kufuatia madai ya baadhi ya watu wasioka waadilifu kutia mchanga laini, maji na mawe kuongeza uzito wakati wakuuza zao hilo linaloiweka Igunga katika daraja la juu nchini.

Alfred Gedi Diwani wa Kata ya Nguvu moja wilayani hapa, amesema kuanzia mwaka 1980 hadi 1990 pamba ya kutoka Igunga ilikua inaongoza Tanzania kwa kuzingatia soko la dunia, hivyo anawaomba viongozi wa AMCOS kuurudisha ubora huo.

Jidashema Mwandu Katibu wa Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae ni Diwani wa kata ya Bukoko wilayani hapa, ameomba siasa chafu kwenye zao la pamba ziwekwe pembeni.

John Leonard Katibu Meneja kutoka Chama cha Ushirika Ipililo kata ya Itunduru, amesema mchanga wakati mwingine unatokana na wakati wanavuna kwa sababu wanaweka pamba chini na hata wanapopeleka nyumbani wanaweka chini.

Aidha, ameshauri  kampuni zinazonunua zao hilo pia zitizamwe kwa sababu zinauonezi na kurudisha lawama kwa AMCOS wakati pamba inaposafirishwa huwa na Mjumbe kutoka AMCOS wanapofikisha kwenye Kampuni wanakagua na kukiri ni safi.

Amebainisha kuhusu vikonyo vinajitokeza kutokana na uvunaji unaofahamika kombakomba ambao huchukua vikonyo, hivyo ameshauri viongozi waendelee kutoa elimu kwa wakulima.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Saud Mtondoo amebainisha zao la pamba ni zao la kimkakati sio tu katika wilaya hiyo ispokua kitaifa, hivyo serikali imekua ikiwekeza nguvu kubwa kuhakikisha tija inapatikana.

Amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia na Waziri wa kilimo, Hussen Bashe kwa sababu wanafanya kazi kubwa ya kulifanya zao la pamba lilete ufanisi na tija kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.

Amedokeza kuwa jitihada zimefanyika kuhakikisha pembejeo, mbegu na viuadudu vinafika kwa wakati ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo inadaiwa msimu ulikua unafika huku pembejeo hakuna, hivyo kusababisha keleke kwa wakulima.

Amefafanua serikali imeendelea kuhakikisha pamba haishambuliwi na magonjwa na kuvunwa ikiwa na ubora hata kwa wale wenye mashamba makubwa wanashindwa kunyunyizia wameletewa vifaa vya kisasa ikiwemo mabodha, ndege nyuki na matrekta.

Ameeleza hatua hiyo iliifanya Igunga kuwa yapili kwa uzalishaji mkubwa wa zao hilo ikitanguliwa na wilaya ya Meatu Kitaifa, hivyo amewaomba waendelee kuwa wachambuzi na wakaguzi wa ubora wa Pamba katika maeneo yao.

Amepiga marufuku kwa AMCOS yoyote kupokea Pamba yenye maji, mchanga au mawe, hivyo watakaobainika kukiuka watachukuliwa hatua kwa sababu watakuwepo wataalamu watakaokua wanapima unyevunyevu ikiwemo mawe na mchanga.

Amesema ni marufuku kwa viongozi wa AMCOS kwenda kupima pamba ya mkulima nje ya kituo cha kununulia pamba huku akisisitiza marufuku kumlipa mkulima kabla ya kuleta pamba kwa makubaliano kwamba atakapovuna ataleta Pamba.

‘’Avune pamba yake iletwe kituoni ipimwe na kukaguliwa ndio alipwe fedha zake kwa sababu ukishamlipa fedha kabla maana yake hata akileta pamba chafu utalazima kuipoeka kwa kuwa fedha yako alikwishachukua na hauwezi kuikataa,’’ amesema.

Aidha, amekumbusha Mkulima atatakiwa kulipwa fedha taslimu kulinga na pamba aliyouza na kupewa risiti kwa sababu serikali imefanya mapinduzi kwa kuleta mizani ya kisasa inayohesabu kila kitu.

Ameeleza mizani hiyo itaambatana na simu janja, printa na sola hali ambayo itapelekea Mkulima kupata risiti na kupata ujembe mfupi kwenye simu yake.

Akizungumzia kuhusu madaraja, DC Sauda ameongeza kutakuwa na madaraja mawili ambayo ni pamba bora na pamba fifi huku bei elekezi ikiwa ni sh. 1150 kwa kilogramu moja ya pamba bora (daraja la kwanza) na sh. 575 kwa pamba fifi.

Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Tabora, Evance Msafiri amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika ya mkoa huo kwenye msimu huu itachukuwa hatua kwa viongozi watakaobainika wameweka mchanga au maji, hivyo watakuwa wamekosa sifa yakuwa viongozi kwa sababu watavunja Bodi yote.

Amezitaka AMCOS kutumia benki mbalimbali kwa kuzipelekea maandiko miradi kwa lengo la kupata fedha za kujenga Maghala ya kisasa huku akiagiza malipo kwa AMCOS na wakulima yafanyike kupitia benki.

Jitihada za serikali ya Rais Dk. Samia katika zao hilo zinatajwa kuendelea kuinua uchumu wa Igunga kwa sababu pamba ndio uchumi wa wilaya hiyo, hivyo nilazima Viongozi, wadau na Wakulima wasimame imara na usimamizi kwa lengo la kuendelea kudumisha  uchumi kwa Halmaashauri na wananchi wake wanaoamini kuwa Pamba ! Dhahabu Nyeupe.

==== //// ==== //// ==== //// ====

Wanufaika wa zao la pamba wilayani Igunga wakiendelea kuchuma pamba kwa lengo la kwenda kuuza (Picha na Hemedi Munga)

Wanufaika wa zao la pamba wilayani Igunga wakiendelea kuchuma pamba kwa lengo la kwenda kuuza (Picha na Hemedi Munga)

Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. Sauda S. Mtondoo akitoa elimu kuhusu zao la pamba (Picha na Hemedi Munga) 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora (Picha na Hemedi Munga)

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA WATAKIWA KUTUMIA KANUNI, SHERIA, TARATIBU NA MIONGOZO KUFANIKISHA UCHAGUZI MKUU 2025

    August 05, 2025
  • RUZUKU ALIYOITOA RAIS DK. SAMIA KWENYE KILIMO YAWANUFAISHA WAKULIMA ZAO LA PAMBA IGUNGA

    March 15, 2025
  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa