Afisa ufatiliaji wa mpango wa TASAF awamu ya tatu katika Wilaya ya Igunga na Nzega Bi.Zahara Omary Mbailwa amewaagiza maafisa Watendaji wa vijiji 54 vinavyonufaika na Mradi wa TASAF III kuwa makini katika kuhakiki taarifa za utimizaji masharti yay a elimu na afya, na kuunganisha orodha ya malipo na namba ya mlengwa wa kaya.
Bi. Zahara Omary Mbailwa ameyasema hayo katika kikao kilichowajumuisha Mratibu wa TASAF III Wilaya ya Igunga na watendaji wa vijiji vinavyonufaika na mradi,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga hivi karibuni.
Afisa ufuatiliaji wa mpango wa TASAF iii ameeleza kuwa lengo la kikao hicho ni kutoa ufafanuzi juu ya vipaumbele vya wanufaika wa mradi wa TASAF awamu ya III na kuwakumbusha watendaji namna ya kuwabaini walengwa ili kuepuka utaratibu mbaya uliojitokeza katika Halmashauri nyingine.
Bi.Mbailwa pia amewatahadharisha watendaji wa vijiji pamoja na wawezeshaji ngazi ya Wilaya kuwa makini pamoja na watoto juu ya utimizaji wa masharti ili kuweza kusaidia Serikali kutopoteza fedha kwa kaya ambazo hazina vigezo.
Jumla ya tarafa nne zenye Kata 35 na vijiji 54 kati ya vijiji 119 katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga vinavyonufaika na Mradi wa TASAF awamu ya III.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa