Serikali Kuu kupitia Mradi wa BOOST imeipatia shule ya Msingi Jitegemee iliyopo Igunga Mjini Shilingi Milioni mia tano na sitini na moja na laki moja (561,100,000) ili kujenga shule mpya yenye Mikondo 16 ( Vyumba 16) na Jengo la Utawala.Shule hiyo mpya ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 720 kwa wakati mmoja.Vyumba vya Madarasa viwili viwili kuanzia Chekechea hadi Darasa la saba.Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe:Dkt Samia Saluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,imedhamilia kuondoa tatizo la miundombinu ya Sekta ya Elimu kwa kutoa Fedha nyingi za Ujenzi wa Mdarasa pamoja na Viti na Meza kwa kila Darasa.Kitendo hiki cha kizalendo cha Rais wetu (MAMA) kimeleta fursa nyingi sana katika Jamii ya Watanzania,ikiwemo Wananchi kupunguziwa ghalama za kuchangia Miundombinu ya Elimu.Pia kuongezeka kwa vyumba vya Madarasa kunatanua wigo wa uhitaji wa Walimu na ndiomaana Mhe; Rais anaendelea kuajiri walimu ili watoto wa Kitanzania wasome na kupata Elimu bora.Majengo ya Shule mpya yapo hatua ya upauwaji na hatua nyingine zinaendelea kwa mfululizo hadi kukamilika kwake.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa