• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

USIMAMIZI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) YA KIPINDI CHA ROBO YA JULAI-SEPTEMBA , 2023

Tarehe iliyowekwa: November 13th, 2023

 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inaendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).

 

 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ambao wanaratibiwa chini ya dawati maalum la Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) lililopo Idara ya Maendeleo ya Jamii lililoanzishwa kupitia “Mwongozo wa Majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii” mwaka 2019.

Usimamizi wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) unatekelezwa chini ya “Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 ikiwa na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 11 ya mwaka 2005 na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 na kufuatiwa na Mwongozo wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara wa mwaka 2020’’.

 

MASHIRIKA YANAYOTEKELEZA MIRADI YAKE KATIKA WILAYA YA IGUNGA

 

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina wadau wapatao 11 ambao wanatekeleza miradi yao katika sekta mbalimbali za Maendeleo hapa wilayani.

Katika idadi hiyo Mashirika sita (6) yanaendelea na utekelezaji wa miradi yao, Mashirika matatu (3) yamemaliza muda wa utekelezaji wa miradi yao na Mashirika mawili (2) wamepokelewa na kutarajia kuanza miradi yao mwezi Oktoba, 2023.

 

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza miradi yake hapa wilayani yamekuwa na mchango chanya katika kuchochea maendeleo kwa jamii zetu kwa kuleta/kusogeza huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazosaidia kupunguza adha na changamoto zinazozunguka jamii hizo.

SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA ROBO YA JULAI-SEPTEMBA, 2023.

Mhe. Mwenyekiti, Katika kipindi cha robo ya kwanza ya Julai-Septemba ya mwaka wa fedha wa 2023 / 2024 Halmashauri imetekeleza yafuatayo:-

  • Imehusisha Kanzidata (database) ya wadau wote wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Miradi yake hapa Wilayani Igunga.
  • Imetoa elimu ya uanzishwaji na usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kupitia mikusanyiko na maombi mbalimbali kutoka kwa jami.
  • Imejengea uwezo na kusaidia mashirika mapya kupata usajili kulingana na Miongozo iliyopo ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).
  •  Imeendelea kuhakiki mashirika yanayotekeleza miradi yake katika Halmashauri hii.

 

 

 

MAFANIKIO 

 katika usimamizi wake Halmashauri imeweza kufanikiwa yafuatayo:-

  • Halmashauri imekuwa na Kanzidata ya Wadau wa Mashirika Iliyohuishwa.
  • Imefanikiwa kuzijengea uwezo Asasi mbili na kuziwezesha kufanya usajili.
  • Kupitia ushirikiano unaotolewa na Halmashauri, wadau wameweza kufikisha baadhi ya  huduma mbalimbali ngazi ya jamii kama vile afya, elimu, msaada wa kisheria nk
  • Mashirika yametengeneza ajira kwa jamii kupitia shughuli zake mbalimbali.
  • Wadau wamepata mwitikio chanya na kuanza kutoa ushirikiano katika mambo mbalimbali
  • Kufanyika kwa vikao vya Wadau na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kama Mwongozo wa Mashirika yasiyo ya kiserikali unavyoelekeza.
  • Kuimarika kwa Mahusiano baina ya Halmashauri, Wadau wa Mashirika yanayotekeleza miradi hapa wilayani na Wawakilishi wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) ngazi ya Mkoa.

ORODHA YA MASHIRIKA YANAYOTEKELEZA MIRADI  YAKE WILAYANI IGUNGA

1. MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI  WANAOENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI 

NA. 

JINA LA SHIRIKA 
MRADI UNAOTEKELEZA 

 JUMLA YA THAMANI YA MRADI  

SEKTA

 MFADHILI 
WANUFAIKA

1

Igunga Paralegal Center (IPC)
Upatikanaji wa Haki Kwa Jamii

  12,500,000.00

Sheria

Legal Service Facility - Tanzania
Makundi Maalum

2

Management and Development of Health (MDH)
Afya Jumuishi

  1,243,000,000

Afya

CDC / PEPFAR
Makundi hatarishi (AYGW) na Makundi Waathirika (PLHIV)

3

Inland Development Tanzania (IDT)
ACHIEVE

  105,592,800.00

Afya

United States Agency for International Development (USAID)
Watoto wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI umri wa miaka 0-17

4

Johns Hopkins Program for International Education in Gynecology and Obstetrics (JHPIEGO)
TOHARA

Afya

United States Agency for International Development (USAID)

USAID AFYA YANGU

Afya

United States Agency for International Development (USAID)
Wajawazito na watoto wachanga , Afya ya Watoto, Lishe, Chanjo, Vijana 10-24.

5

Elizabeth Glasser Pediatric Aids Foundation (EGPAF)
USAID AFYA YANGU-NORTHERN ZONE

      78,452,656.00

Afya

United States Agency for International Development (USAID)
Wagonjwa wa Kifua Kikuu
MALEZI NA MAKUZI

       12,000,000.00

Ustawi wa Jamii

Conrad Hillton Foundation
Watoto chini ya miaka 5

6

Compassion             (Vituo 4 vya Makanisa)
Huduma ya mtoto na Kijana

       37,200,000.00

Jamii

Compassion Tanzania
Watoto na Vijana

2. MASHIRIKA YALIYOMALIZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YAKE  

7

Media for Development and Advocacy (MEDEA)
SAUTI ZETU
    182,000,000.00

Jamii

MALALA FUND
Mabinti

8

National Council of People Living with HIV (NACOPHA)
HEBU TUYAJENGE PROJECT

  20,145,000.00            (kwa mwaka)

Jamii

United States Agency for International Development –(USAID)
Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

9

Jikomboe Integral Development Association (JIDA)
USAID AFYA YANGU

     144,000,000.00

Jamii

USAID - JHPIEGO
Watoto waishio mazingira hatarishi

3. MASHIRIKA YALIYOHAKIKIWA KUANZA UTEKELEZAJI MWEZI OKTOBA, 2023.

10

Thubutu Africa Initiative (TAI)
USAID AFYA YANGU

Jamii

USAID - JHPIEGO

Wanawake , Watoto na Vijana 10-24.

11

BRAC Maendeleo
UWEZESHAJI WA WASICHAN A NA WANAWAKE KIJAMII NA KIUCHUMI

 12,897,721,200.00

Jamii

MASTERCARD FOUNDATION

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WATAKAOWEKA UCHAFU KWENYE PAMBA

    April 22, 2025
  • WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZOTE KARIBU YAO IGUNGA

    March 12, 2025
  • WANAWAKE WAKUMBUSHWA UMUHIMU WAO DUNIANI

    March 09, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa