Wilaya ya Igunga imezindua zoezi la utambuzi na upigaji chapa ng’ombe katika Halmashauri yenye vijiji 119, ambapo zoezi hilo limezinduliwa katika Kijiji cha Igoweko Kata ya Igoweko Tarafa ya Simbo. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh.John Gabriel Mwaipopo akizindua zoezi hilo lililoanza tarehe 01.12.2017 hadi tarehe 31.12.2017 ambapo ndipo litamalizika kwa Wilaya yote ya Igunga ikiwa ni agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga chapa ng’ombe wote wanaopatikana hapa nchini.
Akitoa uhutuba ya Ufunguzi mbele ya mgeni rasmi Afisa Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Dr.Emmanuel Msaki alisema “Wilaya ya Igunga inajivunia kuwa mifugo mingi takribani Ng’ombe 685416, Mbuzi 364252 na Kondoo 195024 , pia aliendelea kusema kuna minada ya awali miwili na mmoja ambao hufanyika kwa wiki mara moja.”
Dr .Emmanuel Msaki aliendele kueleza umuhimu wa zoezi la utambuzi na Mifugo kwa kuwaeleza wafugaji kuwa wataweza kuthibiti wizi wa mifugo yao kwa kuitambua kutokana na Chapa iliyopo kwenye eneo lao kwa kuifatilia kwenye maeneo mbalimbali yya mikusanyiko ya Mifugo mfano Machinjio na Minada.Pia kutasaidia kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya Mifugo kwa kudhibiti mienendo ya Mifugo ndani na Nje ya Nchi.
Alimweleza Mgeni rasmi na wananchi na wafugaji kwa ujumla zoezi hili la utambunzi na Upigaji Chapa Ng’ombe litasimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Idara ya Mifugo na Uvuvi ambapo Afisa Utambuzi,Usajili a Ufuatiliaji wa Mifugo wa Wilaya atasimamia taratibu sheria na kanuni za Utambuzi wa Mifugo. Aliendelea kusema zoezi hili litakuwa na na gharama ya (Tsh.500) shilingi mia tano kwa kila Ng’ombe atakayepigwa chapa ikiwa ni bei elekezi ya Serikali kwa Nchi nzima.
Akimkaribisha Mgeni rasmi Afisa Tarafa Bw.Shedrack Kalekayo pia kaimu Afisa Tawala Wilaya ya Igunga alitumia fuusa hiyo kuwakumbusha wananchi na wafugaji wote umuhimu wa kuwapeleka watoto shule ili mifugo iweze kuwakomboa, pia aliwakumbusha kufatilia mahudhurio ya wanafunzi na kuendelea kuwasisitiza kutokuwagiza au kuwaachia watoto kwenda kwenye “Makomelo” kwani watoto hudumbukia kwa kukosa uangaliza na kupoteza maisha.
Nae Mgeni rasmi Mkuu Wilaya ya Igunga Mh.John Gabriel Mwaipopo akiongea na Wananchi na Wafugaji katika kata ya Igoweko aliwapa faida za utambuzi na upigaji chapa ng’ombe kuwa ni ozezi la Kitaifa ambalo linafanyika Nchi nzima na na niagizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Serikali inahitaji kuhjua idadi ya mifugo iliyopo Nchini, kuiongezea thamani mifugo kwa nyama inayochinjwa hapa Nchini Tanzania iweze kuuzika katika Nchi za Comorro , Asia na Nchi za Ulaya pia kwa kutambulika kwa Mifungo kuwa ni ya Tanzania Ngozi itapanda thamani.
Aliendelea kuwaeleza wafugaji kuwa wataweza kukopeshekaa na taasisi za kibenki kwani mifugo yao itakuwa imetambuliwa rasmi, na kwa kuwa Wilaya ya Igunga inaongoza kwa kwa mifugo hii ni furusa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuanzisha Viwanda vya Usindikaji Nyama ili kuendna na kauli mbiu ya Mh.Rais Dr John Joseph Pombe Magufuri ya Viwanda.
Mh.Mgeni rasmi Mkuu Wilaya ya Igunga Mh.John Gabriel Mwaipopo aliwasisitiza wafugaji kuwa na mifugo yenye tija kwa kujenga nyumba bora, kusomesha watoto na siyo watoto kutumika kuchunga ng’ombe.pia aliwaasa wananchi na wafugaji wa Wilaya ya Igunga kutumia mifugo yao kuchangia chakula mshuleni ili wanafunzi waweze kupata mlo wa mchana waweze kujifunza vizuri kwani mwanafunzi akiwa na njaa hawezi kusoma na kusikiliza mwalimu darsani vizuri.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa