MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mhe.Sauda Mtondoo amewahakikishia wananchi hali ya utulivu na amani katika muda wote watakao kuwa wakitimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
Mhe. Sauda ameyasema hayo leo Jumatano November 27, 2024 baada ya kupiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Jitegemee.
Ameweka wazi kuwa hali ipo salama na tulivu katika vituo vyote vya kupigia Kura kutokana na namna walivyojipanga vyema kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa utulivu na amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambae ni Msimamizi wa Uchaguzi , Bi Selwa Abdalla Hamid ametoa wito kwa wananchi wajitokeze vituoni kupiga kura.
Amewapongeza Wasimamizi wasaidizi katika vituo vya kupigia Kura kwani kwa kufuata taratibu zote za Kupiga kura.
Naye mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Leonsi Mageda ameweka wazi furaha yake ya kutekeleza haki yake ya kimsingi kwa kupiga kura kuchagua viongozi wanaowahitaji.
====////====////====////====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa