Mkagunzi wa hesabu za ndani Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Bwana Abdallah Habibu Mbuyu,mewataka Watendaji wa Serikali za Vijiji kufata taratibu, Kanuni na Sheria na miongozo ya TASAF III katika zoezi la uhawailishaji fedha, alipokuwa katika zoezi la ukaguzi namna zoezi linavyotekelezwa katika vijiji vya Mwabubele, Kalangale, Buchenjegele, Mwamapuli, Chibiso na Mondo Wilayani Igunga.
“Nahitaji kujiridhisha kama fedha zinawafikia walegwa, kuhakikisha kama kuna ushiriki wa wajumbe wa serikali ya kijiji kwenye zoezi zima la uhawilishaji pamoja na wajumbe wa malipo CMC” ameongeza bwana Mbuyu makaguzi wa hesabu za ndani halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
“Nasisitiza Serikali za vijiji kuweka utaratibu madhubuti wa fedha za walengwa zinazochukuliwa na ndugu wa mlengwa mtoto, mjukuu, rafiki aiu mjumbe wa Serikali ya Kijiji na kuhakikisha fedha hiyo inamfikia mlengwa mwnyewe hata kama hajiwezi au ni mgonjwa ili kuondoa malamiko na manunguniko ya walengwa kukosa malipo yao” ameongenza Bwana Mbuyu mkaguzi wa hesabu za ndani halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
“Nafatilia taratibu za uhawilishaji fedha pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za malipo za kila siku za malipo na dirisha lililopita” ameongeza Bwana Mbuyu Mkaguzi wa Ndani Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Bwana Abdallah Habibu Mbuyu akiongea na Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mwabubele, Kalangale, Mwamapuli, Chibiso na Mondo amesisitiza wajumbe wa Serikali ya Kijiji kujiridhisha,kutembelea na kuangalia kama taratibu za malipo zinazingatiwa katika kila dirisha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mondo na Chibiso wamesema kuna changamoto kubwa inayowakabiri ya ukosefu wa watendaji wa vijiji katika vijiji vyao, hali ambayo inasababisha utunzaji wa kumbukumbu za malipo kuwa ngumu, Kwani kukosekana kwa watendaji wa vijiji na uongozi thabiti husababisha kutowewepo kwa kumbukumbu sahihi za malipo wanajitolea kukaimu hujiudhuru mara kwa mara.
Changamoto zinazojitokeza kwenye zoezi zima la uhawilishaji fedha moja ni kuchukuliana fedha kwa wale ambao hawajiwezi kufika eneo la malipo pamoja na wagonjwa.
Pia wajumba wa Serikali ya kijiji cha Mwabubele, Kalangale, Mwamapuli, Chibiso na Mondo wamesema kuna changamoto ya utoro kwa wanafunzi wanaotakiwa kutimiza masharti ya elimu kutokufika shule pamoja na wale wa masharti ya afya kutokupeleka watoto wao kliniki.
Nao walegwa wa TASAF III katika kijiji cha Chibiso na Mondo kata ya Choma wameeleza changamoto wanazokutana nazo pamoja na mafanikio waliyoyapata amabayo ni pamoja na kupata chakula cha kutosha, kupeleka watoto shule na pamoja na kuweza kuchangia matibabu ya CHF.
“Nafuarahia kuwepo kwa Mradi huu wa TASAF III, kwani umeniwezesha kununua nguo na daftari za wanafunzi wanaosoma, Ng’ombe, viti vya kukalia nyumbani pamoja na kondoo watano” Bi, Panki Salawa ameongeza Mlengwa wa TASAF III kijiji cha Chibiso Kata ya Choma.
Bi.Dina Madeje Mratibu wa TASAF III Wilaya ya Igunga,amekiri kuwepo kwa changamoto ya watendaji wa vijiji walio wengi hasa vijiji vile ambavyo vimekaimiwa na wenyeviti wa vitongoji na baadhi ya wataalam katika zoezi la TASAF III, kumekuwa na changamoto ya nyaraka nyingi kutopatikana kwa wakati na utunzaji wake kutokuwa mzuri kutokana na walio wengi kutokujua taratibu, kanuni na sharia za fedha.
Imetolewa na
Kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa