MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Ndug. Hamisi H. Hamisi amekiri kupokea fomu za kugombea ubunge jimbo la Igunga na Manonga za wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Ndug. Hamisi amekiri kupokea fomu hizo leo Agosti 27 , 2025 katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo mjini hapa.
"Nimepokea fomu ya Ndug. Abubakar Alli Omari wa jimbo la Manonga na Ndug. Kabeho Henry Charles wa jimbo la Igunga wa Chama cha Mapinduzi ," amekiri.
Aidha, amewaeleza wagombea hao mchakato wa uteuzi unaendelea na ifikapo saa 10 jioni majina yatasomwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo za Tume hiyo Huru ya Taifa mjini hapa.
Zoezi la kuchukua fomu kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge lilianza Agosti 14 na leo Agosti 27, 2025 ndio mwisho huku wagombea wasubiri uteuzi.
===== ///// =====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa