MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Ndug. Hamisi H. Hamisi amewakabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Igunga na Manonga wagombea wa chama cha CHAUMA.
Ndug. Hamisi amewakabidhi fomu hizo leo Agosti 25, 2025 katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo mjini hapa.
"Ninakukabidhi fomu Ndug. Anthony Kayange Luhende wa jimbo la Manonga na Ndug. Simon Ramadhani Bwiru wa jimbo la Igunga mzijaze na kuzirudisha muda uliopangwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, " amekabidhi.
Aidha, amewakumbusha wagombea hao kuzisoma, kuzijaza na kuzirudisha ndani ya muda uliokusudiwa.
Naye Ofisa Uchaguzi wa wilaya hiyo, John Tesha amesema Wagombea ubunge wa vyama mbalimbali 14 wamechukua fomu ambapo jimbo la Manonga ni Saba na jimbo la Igunga ni Saba.
Zoezi la kuchukua fomu kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge lilianza Agosti 14 na linatarajiwa kuhitimishwa Agosti 27, 2025.
===== ///// =====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa