Bwana Meshack Baraka Opinde, Mhasibu Kituo cha AFya Nanga amewataka walimu wakuu wa shule zote 133 za Serikali Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kufata taratibu, kanuni na sheria wakati wa kufanya malipo kwenye mfumo wa malipo ngazi za kutolea huduma Facility Financing Accounting and Reporting (FFARS), katika shule ya msingi Ziba iliyoko kata ya Ziba tarafa ya Manonga hivi karibuni.
Bwana Opinde aliendelea kuwasisitiza walimu wakuu hao pamoja na walimu wahasibu, kuwa mfumo wa FFARS unakupa mwanya wa kukiri kupokea fedha, kutumia, kutoa stakabadhi, kutoa hati ya malipo pamoja na kuangalia namna ya matumizi yako “Cash Book” yako ya shule.
“Nawaombeni mfate taratibu, kanuni na sheria ikiwa ni pamoja na miongozo inayoletwa na Serikali katika matumizi ya fedha hizo hasa za Elimu Bure,” aliongeza Bwana Opinde.
“Serikali imeleta fedha hizi kwa malengo mahususi hivyo ni vyema tukayafata kama yanavyoelekeza ili kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli, na kumuunga mkono katika juhudi za kuinua taaluma katika shule zetu, na kutokomeza kutokujua kuandika ,kusoma na kuhesabu” aliongeza Bibi Dora Stephen Simbachawene Afisa Elimu msingi Wilaya ya Igunga.
Naye Afisa TEHAMA Wilaya ya Igunga, Bwana Apollo Petro Daudi amewakumbusha walimu wakuu hao, kuwa katika kila shule wamepewa uwezo wa kufanya kazi watu wawili ikiwa ni Mkuu wa shule ambaye ni Msimamizi tu, Mwalimu mhasibu atakayeshiriki katika kuandaa malipo, hivyo atakayekuwa na uwezo wa kufanya malipo ni mwalimu mhasibu tu, Mkuu wa shule ataidhinisha malipo hayo baada ya hati ya malipo kutoka kwenye mfumo.
Mafunzo haya yamefanyika kwa awamu nne kutokana na ukubwa wa Halmashauri na jiographia ya Wilaya yetu, tulianza na tarafa ya Igurubi, Igunga, Simbo na mwisho tunamalizia na manonga ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa fedha ngazi za kutolea huduma (FFARS).
Pia wameomba changamoto zilizopo za kimfumo kutatuliwa na wataalamu pamoja na uongozi, ikiwa ni pamoja na baadhi ya akaunti za shule kukosewa na kusababisha maafisa Elimu kata wengine fedha zao kwenda shule nyingine. Walimu wakuu hao wamekubali kutekeleza aagizo na maelekezo yote kwa kufata taratibu kanuni na sheria zilizowekwa.
Walimu wakuu hao wameshukuru kwa kuwepo kwa mfumo huo wa malipo katika ngazi za kutolea huduma hasa mashule na zahanati yaani Facility Fanancing Accounting and Reporting (FFARS) na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka katika kuwawezesha kushiriki katika kufanya maamuzi katika shule zao.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa