Mhandisi wa maji Wilaya ya Igunga, Mhandisi Christopher Saguda amewataka kamati ya maji kijiji cha Isenegeja, mtendaji wa kijiji na kata kufanya kazi kwa ushirikiano na kujituma katika usimamizi wa mradi wa maji unaojengwa kijijini hapo alipotembelea kukagua maendeleo hivi karibuni.
Mhadisi aliwaeleza wanakamati hao kampuni inayotekeleza Mradi huo ni MONMAR & SONS Co.Ltd ya Mkoani Tabora, Mradi huo unaitwa Isenegeja Water Supply Scheme na utagharimu kiasi cha Tsh.300.526,240.6 milioni.
“Msiposhirikiana ipasavyo mradi huu hamtajua unaendeshwa je? na mtashindwa kuwaeleza wananchi waliowachagua jinsi mlivyoshiriki kusimamia” alisema Mhadisi Christopher Saguda.
Wananchi wa kijiji cha Isenegeja, shule ya Sekondari mwisi pamoja na majirani zao kijiji cha Kalemela watafaidika na mradi huo wa maji ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa tatu 2018. Pia wananchi wamefurahishwa na kusema wako tayari kulinda miundombinu itakayowekwa kwa manufaa ya kijiji na kizazi kijacho.
Pia mradi utakuwa na tenki la kutunza maji la lita elfu sitini (60000), ambalo litakuwa na urefu wa mita 9, litawekewa javi la mita 3.18. Katika shule ya Sekondari Mwisi litawekwa tenki la Polytank la lita elfu kumi (10000), litakalosambaza maji katika bweni la wasichana na wavulana.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa