WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Dk. Dorothy Gwajima ameitaka jamii kubadili mtazamo wanapopita katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii na kufuatilia kurasa za mitando ya serikali kwa lengo la kuelewa namna ambavyo Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alivyoleta maendelo kwa jamii na Mtu mmoja mmoja.
Mhe. Waziri Dorothy ameyasema hayo Ijumaa Januari 10, 2025 wakati akizindua kikundi cha Wanawake kijiji cha Mwanzugi kilichopewa sh milioni 30 na Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Alisema wanapoyapokea hayo maendeleo na kuyatafsiri wasikatishwe tamaa wayataje kwa lengo la kuhakikisha wale wasio kubali kwenda na serikali inapotaka kwenda au watafute njia yao waende wanakotaka kwenda wayaone.
Alieleza kuwa serikali inafikika na ipo kiganjani kwao kidijitali hivyo wasikubali kufangamana na watu wanaowakatisha tamaa kupata stahìki zao za msingi ikiwemo mikopo inayotolewa na serikali.
"Maendeleo wanaweza kuletewa wayasikilize au wayatafute wayaone mfano tangu Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani mkoa wa Tabora uliishapokea zaidi ya sh Trilioni 1.1 kusukuma na kuleta maendeleo ya miradi katika sekta zote " alisema.
Aidha, alisema ni jukumu lao kuyataja maendeleo, kutafuta taarifa zake wanazozitoa kila siku kwa lengo la kupata maneno ambayo watayazungumza kwa watu wanaodaiwa kutotaka kukubali kwamba Mhe. Rais Dk. Samia amefanya maendeleo wasikie na wayaone.
" Ndugu wananchi ! Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anajenga miundombinu ya uchumi mifukoni mwa vikundi na mtu mmoja mmoja ikiwemo Wanaume kupitia Baraza la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi kuna mifuko zaidi ya 100," alisema.
Alidokeza kuwa mwaka 2024, Rais Dk. Samia alianzisha programu inayowagusa sio wanawake tu wakiwemo wanaume wanaofanya biashara ndogondogo.
Aliweka wazi kuwa mkopo huo ulipitishwa na Bunge takribani sh. bilioni 10.5 huku sh. bilioni tano tayari zimeishatolewa kwa lengo la kuona kasi ya kuzikopa kutoka kwenye benki ya NMB ambayo ilishinda zabuni.
Kutokana na hayo, aliwahimiza watafute habari kwenye kurasa rasmi za serikali za mitandao ya kijamii ikiwemo kusikiliza radio na kutazama televisheni kwa kuwa serikali imeendelea kuzindua mikopo mbalimbali ya kuwawezesha Watanzania kiuchumi.
Alibainisha kuwa kunamkopo mwingine wameuzindua mwezi Disemba,2024 kwa lengo la kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dk. Samia kwamba pamoja na mkopo wa asilimia 10 unaotolewa kwenye Halmashauri inchini wazindue mwingine unaoitwa Pamoja Programu utakaoongeza uwezashaji wa Wanawake kiuchumi.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Igunga, Athuman Mdoe alimpongeza Mhe. Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuinufaisha kata hiyo kwa sababu walipata fedha sh. milioni 603 kujenga shule ya sekondari, milioni 561 shule ya msingi na watoto wanasomea huku sh. milioni 361 zimekamilisha madarasa shule ya sekondari Mwanzugi.
Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Mwendo kasi, Telezia Nkamba aliwataka Wanawake kuchangamkia fursa na kuacha tabia ya kukaa kwa sababu sasa hivi sio zama za kanga, vitenge na kuendesha majungu.
"Hatuwezi kufanikiwa tukiwa na majungu ya pembeni , njooni mjifunze tuwasadie la kufanya kwa sisi tuliopiga hatua tuendelee kutafuta maisha na kuisaidia jamii na watoto wetu" alisisitiza.
====== ////// ==== ////// ======
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa