Mkagunzi wa Hesabu za ndani Mwandamizi Wilaya ya Igunga, Bwana Abdallah Habibu Mbuyu, amewataka walengwa wa TASAF III kueleza manufaa waliyoyapata kwa kuwepo katika mpango wa kunusuru kaya masikini wa TASAF III na changamoto wanazokutana nazo wakati wa zoezi la uhawilishaji, akiwa kwenye shughuli za ukaguzi wa pesa za TASAF III, na jinsi pesa wanazopata zinavyowanufaisha katika vijiji vya Bulyangombe,Igumo,Utuja,Mwabakima , Migongwa na Ugaka Wilayani Igunga hivi karibuni.
“Ni lazima siku ya malipo wanakamati wa serikaliya kijiji wanaohusika na TASAF III, pamoja na CMC wote wanaohusika na malipo kusaini kwenye daftari la mahudhurio siku ya uhawilishaji fedha” alisema Abdallah Mbuyu Mkaguzi Mwandamizi Wilaya ya Igunga.
“Tumeunda vikundi sita kwa siku ya leo kwani ilikuwa ndiyo siku ya kuunda vikundi ili kuwaelimisha jinsi ya kujiwekea akiba na kujikwamua kiuchumi kutokana nafedha wanayoipata, na vikundi tulivyoviunda wamechagua majina wenyewe kulingana na vitongoji wanavyotoka ikiwa ni kurahisisha kukutana katikati ya wiki aumwisho wa wiki, vikundi hivyo ni Neema,Upendo,Utulivu,Nguvukazi,Maisha kuona Mbele, Makazi na Muungano” alieleza Bibi Leticia Mihigomwezeshaji wa TASAF III ambae pia ni Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Choma.
Katika kijiji cha Migongwa walengwa wameunda vikundi kumi ambavyo vimeundwa kulingana na vitongoji wanavyotoka ambavyo ni Mtoni–Mwatujara, Ushirikiano, Wapendanao, Imaramakoye-Imaraupina, Upendo,Umoja, Maendeleo, Mwamuhula, Umoja na Nguvu ambavyo vitakuwa vinakutana katikati ya wiki au mwisho wa wiki kujadili shughuli za kiuchumi na biashara kwa kujiongezea kipato.
Walengwa wameeleza kuwa changamoto wanazozipata zaidi niukosefu wa Afisa Ugani wa Kijjiji kwani aliyepo ni wa Kata ambaye anashughulikia eneo kubwa sana la Kata.
Akiongea na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ugaka mkagunzi wa Hesabu za ndani mwandamizi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bwana Abdallah Habibu Mbuyu,amemwagiza Afisa huyo wa kijiji pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji kusoma mapato na Matumizi ya kijiji kwa wanannchi, pamoja na kuwasomea matumizi kwa juu ya mifuko 100 ya Mbunge aliyoitoa ikiwa ni juhudi za kuunga mkono ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ugaka.
Walengwa wa TASAF III, wameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Dr.John Pombe Magufuli (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kwa mafanikio ambayo wameyapata kutokana na kuwepo TASAF III, Wamefanikiwa kununua mahitaji ya shule ambayo yamechochea ari ya watoto wao kwenda shule na kuongeza ufaulu, kumekuwa na ongezeko la mahudhurio ya watoto wa klinik, pia wameweza kuwekeza katika nyanja mbalimbali kama kilimo, mifugo, ujenzi wa nyumba na ushiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya kijiji.
“Naishukuru TASAF III kwa kuniwezesha kupata kuku,Bata na Mbuzi ambao nimewapata kutokana na TASAF III na sasa naweza kupata chakula cha familia yangu, kujiunga na mfuko wa matibabu wa CHF” Bibi Meresiana Mwashi Ruyuga, aliongeza kutoka Kijiji cha Igumo.
Naye Bibi Christina Elias amesema nilianza na kuku watano na Mbuzi mmoja sasa nimeuza nimenunua Mbuzi na Ng’ombe mmoja hata kama ni dume, pia ninauhakika wa kuweza kulima shamba kwani pesa ninayoipata inanisaidia kupata watu wa kunisaidia kulima” aliongeza kutoka kijiji cha Bulyang’ombe kata ya Nanga.
Mkaguzi wa hesabu za ndani Mwandamizi aliendelea kutaka kujua shughuli za walengwa wa TASAF III, za kila siku katika kijiji cha Mwabakima na Migongwa, walengwa walieleza kuwa wanajishughulisha na shughuli za kilimo, biashara ndogondogo na ufugaji (kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe, nguruwe na bata).
Walengwa wameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Dr.John Pombe Magufuli, kuwajali na kuendelea kutekeleza ahadi za ilani ya Chama cha Mapinduzi kama zilnzvyotekelezwa kwa kusimamia miradi inayoendelea kujengwe katika Wilaya ya Igunga.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa