WASIMAMIZI 2,184 wa uchaguzi Mkuu ngazi ya vituo katika jimbo la Manonga na Igunga mkoani Tabora wametakiwa kusimamia uchaguzi kwa weledi unaozingatia taribu na maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Wito huo umetolewa leo Jumapili Oktoba 26, 2025 wakati wa mafunzo elekezi kwa Wasimamizi wakuu na Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika wilaya hiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Msimamizi wa majimbo hayo, Ndug. Hamisi H. Hamisi amefafanua kuwa Wasimamizi Wakuu ni 728 huku
Wasimamizi wasaidizi wakiwa 1,456.
Aidha, wasimamizi hao, wamejifunza majukumu ya watendaji wa vituo, Utaratibu wa kupiga kura na mambo muhimu ya kuzingatiwa kabla, wakati na baada ya kupiga kura, kufunga Kituturu, Sanduku la kura kwa kutumia lakiri na wanaoruhusiwa kupiga kura katika kituo.
Aidha, Mada nyingine ni utaratibu wa kuhesabu kura na makabidhiano ya vifaa na fomu.
Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa zimesalia siku tatu wananchi watimize haki yao ya kikatiba ya kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

==================
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa