MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Igunga na Manonga, Ndug. Hamisi H. Hamisi amewaasa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya kata kuendeleza utendaji wao wa kiuadilifu, uaminifu, uzalendo, uchapakazi na uaminifu.
Ndug. Hamisi ametoa rai hiyo leo Jumatatu Agosti 04, 2025 wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Maxweli mjini Igunga.
“Nyinyi mliopo hapa mmeteuliwa kwa mujibu wa sheria, hivyo mnaowajibu wa kikatiba na sheria kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika maeneo yenu’’ amesisitiza.
Aidha, amewakumbusha wamebeba dhamana kubwa, nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Tanzania Bara, hivyo wanategemewa kuzingatia utendaji wao na kuwajibika ipasavyo kipindi chote cha utumishi wao katika Tume Huru ya Uchaguzi.
Pia, amewataka kufanya mawasiliano na Msimamizi wa Uchaguzi au Afisa Uchaguzi pale ambapo wanahitaji ushauri kuhusu masuala ya uchaguzi.
Kwa upande wa mmoja wa watumishi hao watume ambae ni Mtendaji wa Kata ya Itunduru wilayani hapa, James Samwel amemuhakikishia Msimamizi huyo kuwa timu aliyonayo ni timu bora itakayofanya kazi kwa ufanisi.
‘’ Sisi tunasema hatutakuangusha tunaahidi tuko tayari kwa mafunzo na tutatoa ushirikiano muda wote kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu,’’ amesema.
==== //// ==== //// ==== ///
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa