Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bwana Revocatus L.K.Kuuli amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kufata taratibu,kanuni,sheria na miongozo ya usimamia wa fedha za Serikali wakati wa kukusanya mapato ya Halmashauri kupitia mashine za PoS pamoja na kusimamia ipasavyo miradi ya maendeeo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ya utawala hasa ile ya elimu na afya alipokuwa akizungumza nao katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Igunga hivi karibuni
Ameendelea kuwakumbusha kuwa watendaji wanatakiwa kujua majukumu yao katika maeneo yao ya utawala,pia amewakumbusha kuendelea kupita kwenye miradi hiyo ili kujiridhisha na kazi zinazoendelea hasa kujiridhisha vifaa vilivyonunuliwa.
‘‘Timizeni wajibu wenu,linda heshima ya kazi yako,wewe ndo kiongozi wa eneo lako la kata, simamia ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine ya (PoS)Point of sales’’ameongeza Bwana Revocatus Kuuli, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Igunga
‘‘Leo mmesaini makubaliano haya ambao ndio Mkataba huu unamashsrti tisa kati ya Mwajiri na ninyi Watendaji, najua hizo ni hoja tisa kama hautatekeleza ipasavyo,kanuni zile zile za usimamizi wa fedha za vitabu vya HW5 ndizo hizo zitakazotumika kwangu mimi kama mkaguzi wa ndani nitasimama katika makubaliano haya kama umeyatekeleza ipasavyo, kama utakuwa umeyakiuka taratibu,kanuni,sheria na miongozo ya usimamizi wa fedha utawajibika kwayo’’aliongeza Mkaguzi wa hesabu za ndani Bwana Abdallah Habibu Mbuyu.
Mhasibu wa Mapato amewaasa watendaji wa kata na vijiji mnawajibu wa kukusanya mapato ya Halmashauri kwani Mapato ya Halmashauri yanatokna na mapato yanayopatikana kwenye vijiji na kata zenu.Hii ni kutokana na maagizo ya Serikali ya kuondokana na vitabu vya HW5, mapato yote yanatakiwa kukusanywa kwa mashine isipokuwa mapato mengineyo ya shughuli za maendeleo kwenye Kata zenu.
‘‘Nawataka mjitahidi kuwa waadilifu,kujituma na kujituma najua mnamajukumu mengi na mtapimwa kutokana na ukusanyaji wa mapato kwani maamuzi mengine ya vikao vya madiwani watakuwa wanakuja na hizi taarifa pia vitabu vyote vya HW5 ambavyo havitumiki kwenye makusanyo ya pesa za miradi ya maendeleo kama unavyo virudisheni usije ukapoteza kazi yako’’ameongeza Bwana Nchanana Balele Mhasibu wa mapato Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Pia kwenye maeneo yenu ya kazi kuna matangazo mbalimbali yanatangazwa kwenye kata zenu, matangazo yanatakiwa kuwa na vibali hivyo jitahidi kuona vibali pia wawe na stakabadhi ya mashine.
Imetolewa na Kitengo chaTEHAMA
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
03.06.2019
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa