Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (MB), amewaasa watumishi wa Serikali kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi akiongea nao katika kikao cha kazi cha kufatilia shughulia za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga hivi karibuni.
“unaweza ukawa ni mpenzi wa chama kingine hauzuiliwi, lakini ni muhimu ujue kwamba ndani yako unatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ndiyo chama kinachounda Serikali,na maagizo unayofanya wewe kama mtumishi wa Serikali yanatokana na ilani ya Chama cha Mapinduzi huna sababu yakuonyesha shida ya kutekeleza wajibu wako” alisema Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Ziara hizi zinamadhumuni ya kufahamiana,kukumbushana wajibu na vile vile kuwapa msimamo wa Serikali kujihakikishia kama mambo yanakwenda vizuri” aliongeza kusema Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Jukumu lenu ni kuhakikisha mnawatumikia wananchi wa Igunga, mpo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, wananchi hawatakiwi kulalamika na watumishi mkiwepo katika maeneo haya, Serikali inawaamini watumishi ni wasomi,hivyo ni muhimu kujihakikishia shughuli za kila siku zinaleta mafanikio kwa wananchi wala siyo mafanikio tu na mwananchi anatarajia kuona uwepo wako unatija na lazima uwepo mpango wa kazi wa kila siku, wa robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima.
Alisisitiza watumishi kutumia muda wao kuwatembelea wananchi kujua shughuli zinavyoendelea katika sekta zote za Elimu, Afya, maji,Kilimo na upande wa barabara.Wananchi wanahitaji kujua Halmashauri yao ina mpango gani juu ya Kata na vijiji vyao. Pia aliwaambia shughuli za mikutano ya hadhara si ya wanasiasa tu, bali hata wakuu wa idara wanawajibu wa kufanya mikutano, ili kuwaelimisheni wananchi kujua mipango ya halmashauri yao na serikali yao.Hivyo katibu tawala wa wilaya ni wajibu wake kuwasimamia watumishi ndani ya wilaya, na ndiye mkuu wa watumishi ndani ya wilaya.
Kwa Sekta ya Afya ameagiza kila kijiji kuwa na zahanati, kila kijiji kijenge zahanati yao na Daktari wa Wilaya (DMO) na timu yake ya wataalam ifanye mikakati kupitia mwenyekiti wa halmashauri kwenye mipango ya halmashauri kuhakikisha inasaidia vijiji kwa kuwapatia simenti na bati. Serikali imedhamiria kuona kuanzia ngazi ya kijiji kuna Zahanati.
Kwenye Elimu kunahiatajika kusimamiwa kikamilifu. Mkoa wa Tabora uko nyuma kielimu, maafisa elimu mpo, wasomaji wapo walimu wapo japo hawatoshi, haya yote yanatokana na utoro unaosababishwa na wazazi kupeleka watoto kuchunga mifugo na mimba za utotoni. Ni jukumu la sekta ya Elimu kusimamia na kuyakemea haya kwani yanasababisha elimu kushuka.
Katika Mkutano wa hadhara viwanja vya manadani Igunga Mhe. Waziri Mkuu alisema ”Utumishi wanaotakiwa kutoa siyo ule wenye dalidali za usumbufu kwa wananchi nimekemea tabia ya njoo kesho njoo kesho njoo kesho maofisini tunaamini wale ni wasomi wamesoma vizuri kwenye maeneo yao waliyoajiliwa” aliongeza Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB), ameendelea kuwakumbusha watumishi kujituma na kusimamia kazi zao kwani wameletwa kwa makusudi katika eneo hili la Igunga, kuwatumikia wananchi na wamebobea kwenye taaaluma zao.Na watumie muda wao kuwatembelea wananchi vijijini kufatilia maendeleo ya miradi inayoletwa na serikali.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa