MKuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani, amesema Mkoa wa Tabora umepokea Jumla ya shilingi Billion 46 na Milioni 200 kwa ajili ya kujenga Shule 12 katika Wilaya za Mkoa wa Tabora zenye Madarasa ya kuanzia awali hadi Darasa saba (7) Madarasa yenye mikondo miwili miwili kwa hiyo Shule hizo zitakuwa na jumla ya Vyumba vya kusomea 16 kila Shule.
Pia Dkt Buriani amesema kwa upande wa Sekondari Mkoa umepata fedha za kujenga Shule 12 mpya za Sekondari zenye kidato cha kwanza hadi cha nne (4), na Shule moja ya Bweni ya Umahiri ya Sayansi kwa Wasichana inayojengwa Wilaya ya Kaliua.
Mkuu wa Mkoa alieleza mafanikio makubwa sana ya ufaulu wa matokeo ya Kidato cha sita (6) 2023, kuwa wanafunzi wote waliofanya Mtihani wa Kidato cha 6 Mkoa wa Tabora wamefaulu kwa asilimia 99.99, lakini kipekee Dkt Buriani ameipongeza Halmashauri ya Igunga kuwa na asilimia 75 ya ufaulu wa Daraja la kwanza kiwilaya na kwamba Wilaya ya Igunga hakuna ufaulu wa daraja la nne (4). Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo katika Shule ya Sekondari Mwisi wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilayani Igunga 14/07/2023.
Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha 5 Mkoa wa Tabora kuwa Mwaka jana 2022 walikuwa Elfu mbili na Mia nane tu (2,800), lakini mwaka huu 2023 watakao anza kidato cha 5 ni Elfu sita na kumi na nne (6,014) kuwa ni ongezeko kubwa linalotokana na Matunda ya Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mhe; Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji mkubwa sana katika sekta ya Elimu.
Baada ya kuhitimisha maelezo yake Mkuu wa Mkoa alitoa Maagizo ya Mkoa katika wilaya zake kuwa Kila Halmashauri ihakikishe watoto wote wanaoanza darasa la kwanza wanamaliza darasa la saba (7) kusiwe na mdondoko wa wanafunzi kuishia madarasa ya katikati.Pia aliagiza kila Mzazi achangie chakula cha watoto Shuleni, Serikali za vijiji ndio zitasimamia chakula cha watoto Shuleni.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa