Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr. Charles Msonde amefanya Vikao kazi katika wilaya ya Igunga lengo likiwa ni Kuwakumbusha Walimu majukumu yao na Kuwaeleza Juhudi za Serikali katika kuhakikisha Masirahi ya Watumishi.
Vikao kazi hivyo vimefanyika Juni 11, 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ziba na Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St.Margaret Maria Alakoki Mjini Igunga.
Msonde ameelekeza mambo mbalimbali ikiwemo, Walimu kulipwa Stahiki zao, Kupandishwa madaraja (Mseleleko ), Malimbikizo na hela za likizo kutolewa kabla ya kwenda Likizo.
Vile vile amewasihi walimu kuwa wabunifu katika kuwafanya watoto wapende shule pia kuondoa Daraja F hiyo ikichagizwa na Walimu kupendana wao kwa wao kwani Kwasasa Rafiki wa Mwalimu ni Mwalimu.
Kwa Upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga Ndg. Benjamin Siperto amesema Maelekezo yaliyotolewa ameyapokea na yanaanza kufanyiwa kazi haraka iwezakavyo.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa